|
|
MICHUZI BLOG

MICHUZI


RAIS MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA PASAKA KANISA LA KKKT LA AZANIA FRONT JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Posted: 27 Mar 2016 07:10 AM PDT

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa alipowasili kwa Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mkewe Mama Magufuli wakishiriki na waumini wengine Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini huku akisikilizwa na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa na Mchungaji Chalres Mzinga baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Mama Rebecca Malasusa na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akiwapungia waumini baada ya  Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akisalimiana na mtoto Javiera Lyimo (9) anayesoma darasa la tano shule ya Genesis jijini  baada ya  Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016. 

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Posted: 27 Mar 2016 12:23 PM PDT


SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Generali mstaafu Ezekiel Kyunga awataka mabalozi wa nyumba 10 kuimarisha ulinzi katika maeneo yao kwa kuwa wako karibu sana na makazi ya wananchi. https://youtu.be/CTup2l1P9v4

 SIMU.TV: Wadau wa elimu wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wachangia na kuahidi zaidi ya shilingi milioni 5 za madawati pamoja na mifuko 10 ya simenti ili kunusuru wananfunzi 800 wanaokaa chini. https://youtu.be/5_aLHkI8Hsg

SIMU.TV: Waziri Luhaga Mpina aipa NEMC siku 7 kuibana Dawasco kukomesha utiririshaji wa maji taka kwenye mitaro ya maji ya mvua.https://youtu.be/k9nTECX2628  
   
SIMU.TV: Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam juu ya ujenzi wa barabara ya Makumbusho hadi Mwananyamala laanza kuzaa matunda baada ya mkandarasi kuendelea na ukarabati. https://youtu.be/nl387NcTwF0  
  
SIMU.TV: Wakazi wa kijiji cha Amani wilyani Nanyumbu mkoani Mtwara wagomea kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF baada ya kudai awali kupewa kadi zilizoisha mda wake. https://youtu.be/W9mPI3UClZY  
   
SIMU.TV: Wadau mbalimbali wa elimu jijini Dar es salaam waendelea kutoa misaada mbalimbali kusaidia ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi ya Maji Matitu iliyoko Mbagala kutokana na kufurika kwa wanafunzi. https://youtu.be/BF8vzHAqkb8

TAMASHA LA PASAKA LAPAGAWISHA MASHABIKI WA MUZIKI WA INJILI CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA

Posted: 27 Mar 2016 02:01 PM PDT

11
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiongoza na viongozi mbalimbali pamoja na baadhi ya maaskofu kucheza wakati mwimbaji Upendo Nkone alipokuwa akiimba jukwaani.
12
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipiga picha ya pamoja na waimbaji wa muziki wa injili mara baada ya tamasha hilo kumalizika kutoka kulia ni Bonny Mwaiteje. Jesca BM na Upendo Nkone.
13
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akicheza wakati mwimbaji Bonny Mwaiteje alipokuwa akitumbuiza.
30
Mwimbaji Christopher Mwahangila akiwapa upako mashabiki kupitia injili ya uimbaji.
33
Mwimbaji Ephraimu Sekereti kutoka nchini Zambia naye akaimba nyimbo za kusifu na kuabudu.
34
Solomon Mukubwa akiafunga kazi na nyi,bo zake kali zilizowafanya mashabiki kuwa wima wakati wote kama wanavyoonekana.

TFF YATHIBITISHA KUJITOA KWA CHAD KATIKA MICHUANO YA AFCON 2017

Posted: 27 Mar 2016 10:00 AM PDT

Shirikisho la Soka nchini TFF  limethibitisha taarifa yetu ya awali  kwamba timu ya Taifa ya Chad  ‘Les Sao’ (pichani) imejiondoa katika michuano ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) itakayofanyika mwaka 2017 nchini Gabon.

Tovuti ya TFF inasema kwamba taarifa ya kujitoa kwa Chad imetolewa na Shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika (CAF) leo baada ya Les Sao kuandika barua ya kujitoka katika mashindano hayo ikiwa katika kundi G pamoja na timu za Tanzania, Nigeria na Misri.

Chad ilitarajiwa kucheza kesho Jumatatu dhidi ya Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ikiwa ni mchezo wa marudiano wa kundi G baada ya kucheza mchezo wa awali jijini N’Djamena katika ya wiki.
Katika mchezo wa awali uliochezwa uwanja wa Idriss Mahamat Ouya, Taifa Stars iliibuka na ushindi wa bao 1- 0 , bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta dakika ya 30 ya mchezo.

Kufuatia kujitoa kwa Chad, matokeo ya michezo yote iliyoihusisha timu hiyo yanafutwa, na msimamo wa kundi G kwa sasa unaongozwa na Misri yenye pointi 4, Nigeria pointi 2 na Tanzania pointi 1.

kipa wa zamani wa simba toka uganda Abel Dhaira afariki dunia

Posted: 27 Mar 2016 09:49 AM PDT


Klabu ya Simba imepokea kwa mshtuko taarifa ya msiba wa mchezaji wake wa zamani mganda Abel Dhaira.
Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na mitandao mikubwa ya Uganda ikiwemo ya gazeti mashuhuri nchini humo la New Vision.
Mchezaji huyo aliyekuwa akichezea nafasi ya golikipa na ambae alipata pia kuichezea timu ya taifa ya Uganda.alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya utumbo.
Kwetu sisi ni pigo kubwa sana na msiba mzito sana.umetufanya tupate fadhaa kubwa.lakini hatuna la kufanya.zaid ya kumtakia mapumziko mema ya milele.
Dhaira anakumbukwa sana na wana Simba hasa kwa uwezo wake wa kudaka krosi na nidhamu yake iliyokuwa mfano kwa wachezaji wote waliokuwepo kipindi kile..
Tunawaomba familia ya marehemu iwe na subira kwenye kipindi hiki kigumu sana kwao

Imetolewa na
Haji S Manara
Mkuu wa habari Simba sports club

Machi 27, 2016

mdororo wa kiuchumi Chad wafuta mchezo wa timu ya nchi hiyo na Taifa Stars kesho

Posted: 27 Mar 2016 09:39 AM PDT

CHAMA cha soka nchini Chad FTFA kimetuma barua kwa CAF na TFF kuelezea kushindwa kwao kusafiri kuja nchini Tanzania kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' uliopangwa kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Sababu ya kushindwa kwao kusafiri kama ilivyoelezwa kwenye barua hiyo ni nchi hiyo kuathiriwa na mdororo wa kiuchumi. Ifuatayo ni tafsiri fupi ya barua hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya kifaransa.

"TAARIFA YA CHAD KWA CAF NA TFF
Timu yetu haiwezi kusafiri hadi Dar kwa mechi ya tarehe 28
Nchi yetu imeathirika na mgogoro wa uchumi duniani...hivyo ushiriki wetu kwenye mashindano mbalimbali umepata pigo kubwa kutokana na ukosefu wa fedha.
Tunaomba radhi kwa usumbufu huu ambao ni nje ya uwezo wetu na nia yetu"

Mwakilishi Maalum wa AU kuhusu Libya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Afanya Mazungumzo na Waziri wa Nchi Anayeshughulikia Mambo ya Nje na Mgogoro wa Libya Dkt. Anwar Mohamed Gargash Al-Awadhi wa UAE jijini Dubai Leo

Posted: 27 Mar 2016 07:59 AM PDT

 Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika kuhusu Libya Rais Mstafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokelewa na Mwenyeji wake Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje Mhe Dkt. Anwar Mohamed Gargash Al- Awadh ofisini kwake Dubai
Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika kuhusu Libya Rais Mstafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa UAE Dr. Anwar Mohamed Gargash Al- Awadhi ofisini kwake Dubai.

In loving memory

Posted: 27 Mar 2016 07:45 AM PDT

Dr. Henry C. M. M. Nyamubi 13.02.1958 ~ 28. 03. 2015

A great husband, father, son, brother, uncle, grandfather and friend.

You are physically gone but spiritually ever present. We will never forget your kindness, wisdom and your selflessness in assisting others despite personal difficulties you were going through.

Words, however kind, cannot mend the loss we feel. However we rejoice knowing that you are now with our Lord Jesus and that we will meet again when He calls us.

Thanks Givin mass will be at st Batholomew Anglican Church Ubungo 16:00 Pm.

NAVY KENZO WATUA BUKOBA TAYARI KWA SHOW YAO USIKU HUU LINA'S NIGHT CLUB

Posted: 27 Mar 2016 07:40 AM PDT

Wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo, Nahreel na Aika leo wametua Bukoba ikiwa ni mwendelezo wao wa "Kamatia Chini lights up Tour" ambapo usiku huu watashusha show yao ya Nguvu kwenye Ukumbi wa Burudani wa Lina's Night uliopo Bukoba Mjini. Wasanii hao wanaletwa hapa Mjini Bukoba kupitia kampuni ya Sleek Events ya Jijini Mwanza.
Msanii Aika akishuka kwenye ndege leo hii kwenye Uwanja wa Ndege Mjini Bukoba
Wadau wakipata picha ya pamoja na wasanii wa Kundi la Navy Kenzo

Kushoto ni Mr. Tega JassonMkurugenzi wa Sleek Events akitokelezea kwenye picha ya pamoja na msanii Aika, Faustine Ruta wa Bukobasports.com na kulia ni Bwogi.

Embarking on information technology can reduce congestion and air pollution in our cities.

Posted: 27 Mar 2016 06:59 AM PDT


By Abdalah Kileo
Many jobs, businesses and other activities are drawn into city centers, you can find shops, restaurants, financial services, Government ministries, libraries, colleges, open spaces and other facilities all concentrated in a city centers. 
Since very few people lives in the city center, most of those surrounding the city centers have to access the city through walking, bicycles, motorcycles, public and private cars for their daily activities. This has led to sometimes intolerable levels of traffic congestion on urban streets as well as the main road accessing the city, causing delays and severely effect on productivity of business, their ability to innovate and business access to new markets and resources. 
The problem of congestion span from the business to people who live in our city, they finds themselves stuck in traffic when they should be at work or school and sometimes frustrated at the time wasted in trying to get from point A to point B. 
The problem go far where it increases oil consumption  and CO2 emissions as well as noise emission from transport, with people living along congested routes and very busy towns like Dar Es Salaam they suffer from poorer air quality for most of their life. 

STARS KUWAVAA CHAD KESHO TAIFA

Posted: 27 Mar 2016 06:40 AM PDT

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kesho inashuka dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakabili Chad katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2017.

Taifa Stars itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0 ilioupata katikati ya wiki jijini N’Djamena katika uwanja wa Idriss Mahamat Ouya, bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta dakika ya 30 ya mchezo.

Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema maandalizi kwa kikosi chake yamekalimika, vijana wote wapo katika hali nzuri ya kusaka ushindi ushindi kesho, kikubwa amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Taifa kujwa kuwapa sapoti vijana watakapokuwa wakiwakilisha Tanzania.

Kuelekea katika mchezo huo, tiketi za mchezo zimeanza kuuzwa leo katika vituo vya Ubungo Oilcom, Buguruni kituo cha mafuta, Mbagala Darlive na Karume ofisi za TFF. Viingilio vya mchezo huo ni Shilingi 25,000 kwa VIP A, Shilingi 20,000 kwa VIP B na Shilingi 5,000 kwa viti vya rangi ya Blu, Kijani na rangi ya Machungwa.

ZUBEIR MAULID ACHUKUA FOMU YA KUWANIA USPIKA BARAZA LA WAWAKILISHI, ZANZIBAR

Posted: 27 Mar 2016 02:52 AM PDT

KATIBU wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dk. Yahya Khamis Hamad (kushoto) akimkabidhi fomu ya kugombea uspika, mgombea wa nafasi hiyo kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Zubeir Ali Maulid , ambapo uchaguzi wa spika unatarajiwa kufanyika tarehe Machi 30 , 2016, fomu hiyo alikabidhiwa katika ofisi ya katibu wa baraza ziliopo Mbweni Wilaya ya Magharib ‘B’.
KATIBU wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dk. Yahya Khamis Hamad (kushoto) akisalimiana na mgombea wa nafasi ya Uspika wa Baraza hilo kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Zubeir Ali Maulid wakati alipofika kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo katika ofisi ya katibu wa baraza ziliopo Mbweni Wilaya ya Magharib ‘B’.
MGOMBEA wa Nafasi ya Uspika kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) Zubeir Ali Maulid akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uspika wa Baraza la Wawakilishi katika ofisi za Baraza hilo ziliopo Mbweni Wilaya ya Magharib ‘B’.Picha na Haroub Hussein

SERIKALI YA TANZANIA HAINA MPANGO KWA KUTEKETEZA MENO YA TEMBO YALIYOHIFADHIWA

Posted: 27 Mar 2016 12:59 AM PDT

Serikali ya Tanzania imetoa tamko kuwa kwa sasa haina mpango wowote wa kuteketeza meno ya tembo yaliyohifadhiwa ambayo yametokana na vitendo vya ujangili na vifo asilia vya tembo.

Tamko hilo limetolewa hivi karibuni na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark Childress alipotembelewa na balozi huyo ofisini kwake kujadili maendeleo ya sekta ya Maliasili mchini.

Prof. Maghembe alisema hayo baada Balozi huyo wa Marekani hapa nchini kutoa pendekezo kwa Serikali ya Tanzania kuchoma sehemu meno ya tembo yaliyohifadhiwa ili kutoa ujumbe mzito duniani juu ya dhamira ya Serikali kukomesha biashara hiyo haramu.

"Naomba niweke wazi kuwa kwa sasa hatupo tayari kuteketeza meno haya, tunaweza kuyatumia kwenye tafiti za kisayansi au vielelezo kwa ajili ya kesi za ujangili ambazo zipo mahakamani na nyingine ambazo bado zinafanyiwa uchunguzi" Alisema Prof. Maghembe.

Zipo nchi mbalimbali duniani ambazo zimechukua hatua ya kuteketeza meno yake ya tembo yaliyohifadhiwa ikiwemo nchi jirani ya Kenya na Malawi ambapo inaaminika kuwa kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kushawishi Ulimwengu kukomesha biashara hii haramu ya meno ya tembo.

Nchi nyingine ni Chad, Ubelgiji, Ufaransa, China, India, Marekani na Ureno. Kwa upande wa nchi ambazo zina msimamo sawa na Tanzania katika kuendelea kuhifadhi meno yake ya Tembo ni pamoja na Afrika ya Kusini, Botswana na Zimbabwe.

Akizungumzia kuhusu kuendeleza sekta ya Maliasili nchini, Prof.Maghembe amemuomba Balozi wa Marekani Bw. Mark Childress kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukuza sekta hiyo kwa kuleta wawekezaji mbalimbali kutoka Marekani kuja kuwekeza Tanzania pamoja na kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Ujangili.

Aliongeza kuwa Tanzania ina fursa nyingi ambazo zinahitaji uwekezaji mkubwa ikiwemo hoteli za kitalii, fukwe za kisasa na kuendeleza vivutio mbalimbali vilivyomo hapa nchini.

Prof. Maghembe amemshukuru balozi huyo kwa misaada mbalimbali kutoka Serikali ya Marekani ya kuendeleza sekta ya Maliasili nchini ukiwemo wa hivi karibuni wa mbwa maalum (Snifer Dogs) kwa ajili ya kusaidia utambuzi wa rasilimali za Maliasili zinazoweza kutoroshwa nje ya nchi kupitia bandari na viwanja vya ndege.

Katika taarifa iliyowasilishwa kwenye kikao baina ya Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark Childress imeonesha kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Serikali ya Marekani imetoa misaada mbalimbali ambayo jumla yake ni dola za kimarekani Milioni 41.35 katika kusaidia eneo la uhifadhi hapa nchini.Akizungumzia mahusiano baina ya Tanzania na Marekani Balozi Mark Childress alimueleza Prof. maghembe kuwa Serikali ya Marekani itaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi hizi mbili ambapo pia ofisi yake ya ubalozi imeshatafuta wadau mbalimbali ambao wapo tayari kusaidia fedha, vifaa na mafunzo kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi na mapambano dhidi ya ujangili. 
(Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)

SIMU TV: MAPITIO YA MAGAZETI LEO

Posted: 27 Mar 2016 12:29 AM PDT

Ngoma Africa Band Yawatakieni Heri ya Sikukuu ya Pasaka!

Posted: 26 Mar 2016 09:07 PM PDT


Bendi yako maarufu ya muziki wa dansi “Ngoma Africa Band” aka FFU yenye makao yake nchini Ujerumani, Inawatakieni wadau wote popote pale mlipo KILA LA HERI NA FANAKA katika sikukuu ya msimu wa Pasaka. bendi yenu “Ngoma Africa band” inawaombea amani na baraka. Pia msikose kupata burudani kamili ya Pasaka kwa kusikiliza nyimbo aka (Virungu vya FFU) at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com,
mawasiliano at contact@ngoma-africa.com.
 Gwaride kali
 FFU Ughaibuni kazini
 Hapa kazi tu!
Kikosi kazi
Nyomi

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: k.sher feat squezer - uvumilivu

Posted: 26 Mar 2016 08:00 PM PDT

5.57Score
Be the first to
mark Beautiful

Email Newsletter

Sign up for our email newsletters

Facebook Page

Twitter Page

Recent Post

Tags