|
|
MICHUZI BLOG

MICHUZI


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi atembelea Manyara

Posted: 05 Sep 2016 01:10 PM PDT

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Melania Sangeu akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Manyara Eng. Bashiri Rwesingisa alipokagua usalama wa mazingira katika miradi ya ujenzi wa barabara mkoani Manyara.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usalama na Mazingira(mazingira), wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Melania Sangeu akitoa maelekezo kwa Eng. Peter Bululu ambaye ni mhandisi wa miradi ya barabara mkoani Manyara katika eneo la mpaka wa mkoa wa Manyara na Singida alipokagua usalama wa mazingira ya barabara hiyo. 

 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usalama na Mazingira(mazingira), wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Melania Sangeu akitoa maelekezo kwa Eng. Peter Bululu ambaye ni mhandisi wa miradi ya barabara mkoani Manyara kuhusu umuhimu wa kutochimba mawe na mchanga katika meneneo yaliyo karibu na miundombinu ya barabara, umeme, mwasiliano na maji ili kulinda usalama wa watu, mazingira na miundombinu yenyewe.

Wakazi wa Bombab-Katesh Hanang mkoani Manyara wakibomoa mwamba ili kushusha mawe katika eneo la machimbo ya mawe ambalo ni hatari kwa afya ya mazingira na usalama wa watu.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 05/09/2-16

Posted: 05 Sep 2016 12:52 PM PDT

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Posted: 05 Sep 2016 12:22 PM PDT

SIMU.TV: Naibu waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi William Ole Nasha, amesema serikali ya Korea na Tanzania zimedhamiria kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya kilimo nchini;https://youtu.be/mlhJzUfY1d0

SIMU.TV: Mamlaka ya hali ya hewa nchini imetoa tahadhari ya uwepo wa mvua za chini ya wastani kutokana na kuwepo kwa joto la kawaida katika bahari ya Pacific;https://youtu.be/stppZ6SC35k

SIMU.TV: Mkutano wa nne wa bunge la 11 unatarajia kuanza siku ya kesho mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine, miswada mbalimbali itajadiliwa baada ya kufanyiwa kazi na kamati; https://youtu.be/Clfvlo525SU

SIMU.TV: Katika kutekeleza agizo la Rais kuhamia mkoani Dodoma, wizara ya nishati na madini imeongeza nguvu ya umeme mkoani humo ili kukidhi ongezeko la watu;https://youtu.be/f7YF9TC8N6I

SIMU.TV: Sekretarieti ya jumuiya ya wazee chama cha wananchi CUF visiwani Zanzibar limepinga maamuzi yaliyofanywa na wazee wa jumuiya hiyo walioko Tanzania bara;https://youtu.be/DrlyoPXTtjE

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mwamvua Mrindoko, ameongoza mamia ya wakazi wa wilaya hiyo kwenye mazishi ya watoto 6 waliofariki jana katika ajali ya moto;https://youtu.be/ygtTM0w09nY

SIMU.TV: Waziri wa viwanda, biashara na uwezekezaji Charles Mwijage amewataka watanzania kutumia bidhaa zilizotengenezwa na viwanda vyetu vya ndani;https://youtu.be/VI3-nfoVU2k

SIMU.TV: Benki ya maendeleo nchini TIB imesaini mkataba na benki ya Posta ili kuwawezesha wateja wa TIB kupata huduma za kibenki kupitia benki ya Posta;https://youtu.be/W6yhCbzSgqQ

SIMU.TV: Benki ya KCB imetoa msaada wa shilingi milioni 75 kwa taasisi ya saratani ya Ocean Road ili kuweza kusaidia ukarabati wa hodi; https://youtu.be/VNppYeGTFKU

SIMU.TV: Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuwahimiza watoto kupenda masomo ya sayansi ili kuweza kuongeza watalaamu wa sayansi nchini;https://youtu.be/Up0Xg5NaAMI

SIMU.TV: Makocha 26 wanaoshiriki kozi ya ukocha inayoratibiwa na shirikisho la mpira dunia FIFA wametakiwa kutumia ujuzi walionao kuendeleza soka la wanawake;https://youtu.be/f8RfAogDXS4

SIMU.TV: Chama cha mchezo wa Gofu nchini kimetakiwa kuimarisha mchezo huo kwa wanawake ikiwa ni pamoja na kupata viongozi wake; https://youtu.be/n3g_AGNdacg

SIMU.TV: Mabondia Mohamedi Matumla na Deo Samuel wametambiana kuibuka na ushindi kila mmoja katika pambano lao litakalofanyika mwishoni mwa mwaka huu;https://youtu.be/L5O1Csr1iZw

TEASER JOTO LA ASUBUHI SEPTEMBER 6 JUMANNE

Posted: 05 Sep 2016 12:19 PM PDT

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE KUPIMA WATOTO WENYE MATATIBIZO YA MOYO BURE

Posted: 05 Sep 2016 11:54 AM PDT

Na John Stephen, MNH
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo imeanza kupima watoto bure ili kubaini kama wana matatizo ya moyo watachangia gharama za upasuaji. 
Wazazi na walezi wenye matatizo ya moyo wamejitokeza kwa wingi leo katika taasisi hiyo wakiwa na watoto na kupatiwa vipimo ili kubaini matibabu. 
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi amesema kwamba watoto watakaobainika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa upasuaji.
“Watoto watakaobainika kuwa tatizo tutawafanyia upasuji, wazazi wanatakiwa kuchangia kiasi cha fedha ili kukamilisha matibabu kwa watoto husika,”amesema Profesa Janabi.
Taasisi hiyo imeanza shughuli ya kuwapima watoto ili kubaini kama wana matatizo ya moyo na kuwafanyia upasuaji. Pia, watu wazazi wametakiwa kujtokeza kwa ajili ya watoto kufanyiwa upasuaji.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto katika chumba cha Dk Stella Mongella wakisubiri watoto wao kufanyiwa vipimo Leo kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Baadhi ya wazazi na walezi wakisubiri kuingia kwenye chumba cha daktari kwa ajili ya watoto kuchunguzwa kama wana matatizo ya moyo. Watoto watakaobainika watafanyiwa upasuaji na wazazi watatakiwa kuchangia gharama.
Leo Dk Sulenge Kubhoja wa taasisi hiyo, akimchunguza mtoto Lisa Mashauri (2), mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Dk Sulenge Kubhoja akiendelea na uchunguzi kwa mtoto Hellen Emmanuel kutoka mkoani Iringa.
Baadhi ya wazazi na walezi wakiwa na watoto wao leo nje ya taasisi hiyo kabla ya kuingia katika chumba cha daktari leo.

BENKI YA MAENDELEO YADHAMINI SHINDANO LA GOSPEL STAR SEARCH

Posted: 05 Sep 2016 09:23 AM PDT

Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Benki ya Maendeleo, Peter Tarimo akisaini mkataba wa udhamini wa shindano la Gospel Star Search (katikati) huku meneja wa Mrado huo wa GSS, Samwel Sasali (kushoto) akishudia tukio hilo lililofanyika leo hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam. Siku Ya Leo Kamati Ya Gospel Star Search na Kampuni 2.....Maendeleo Bank na Grace Product Wametiliana Mkataba wa Udhamini wa Gospel Star Search 2016. Pichani tukio likifanyika Regency Hotel. Milango ipo wa Wadhamini wengine Pia Makampuni na watu Wa Mavazi Mnakaribishwa. Meza kuu. 
 Ndugu waandishi wa habari tunashukuru sana kwa kuitikia wito wetu siu ya leo, katika project hii kubwa inayoendelea ya Gospel star search. Tulikwisha kuanza toka na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa mpaka sasa lakini lengo kuu hasa la uwepo wetu hapa siku ya leo ni kuwajuza juu ya uwepo na kutiliana saini na wadhamini wetu ambao wameona ni vyema na tumekubaliana kufanya kazi pamoja katika project hii ya Gospel star search. Nitamkaribisha mwenzangu yeye atasema zaidi kuhusu GSS na hatua tuliofikia mpaka sasa na kuwatambulisha wadhamini wetu.

 LENGO KUU Ahsanteni sana waandishi wa habari kwa kuitikia wito wetu, kama alivyosema mwenzangu lengo letu siku ya leo ni kuwatambulisha wadhamini wetu kwenu na kwa watanzania ,lakini kabla ya kwenda mbali ni vyematukatoa mrejesho mfupi juu ya GSS ilipoanza mpaka hatua tuliofikia kwa mwaka huu. 

 GSS ina lengo kubwa ya kutafuta waimbaji wa muzii wa injili na kuwasaidia kujitambua kuwapa nafasi ili kukuza vipaji vyao na kuvifanya vionejkane kwa watu kwaajili ya kua faida kw watu lakini hata kwao wenyewe pia.Tunaamini sana kipaji kama kikitumika kwa namna ilio sawa kinaweza kubadili kabisa maisha ya mtu na akawa mtu mwingine mwenye maisha bora yalioletwa na kipaji au talanta alionayo hii ndio sababu tumeipa kauli mbiu ya KIPAJI CHAKO…

 HATMA YAKO. Tumeanza na wilaya tatu za mkoa wa Dar es salam kwa sasa, Kinondoni, Temeke pamoja na Ilala na kila sehemu tumechua washiriki wa tano hivyo kua na jumla ya wshiriki 15 kwa wilaya zote 3 ambao hawa ndio wamefanikiwa kuingia hatua ya nuusu fainali. Mchakato wetu umekua na round mbili (2) za mchujo ambazo kwazo ndizo zimetupa washiriki hawa 15 waliopo mpaka hivi sasa. 

 Ndugu waandishi wa habari tunashukuru sana wadhamini wetu ambao waliona ni vyeama kushiriki na sisi kwa kutufanyia udhamini kwenye project hii kubwa ya GSS, ambao leo tuko nao hapa kwaajili ya kuwatambulisha rasmi kwenu..ambao ni • Maendeleo Bank • Grace Product • Brand exponetial

 • Kiango media • Clouds Media Group • Fm studios (Faith music lab) • 3D Kwa hiyo uwepo wetu hapa ni kuwatambulisha rasmi watu hawa amabao wameona ni vyema kusimama na sisi na pia kutiliana saini mbele yenu kama ishara ya kuingia ubia katika project GSS. Kwa kusema haya sasa nitatoa nafasi kwa wadhamini kusema kdogo ju yao lakini pia juu ya GSS karibuni sana!

 HITIMISHO Pia tungependa kuchukua fulsa hii kutoa wito na hamasa kwa makampuni mengine ambao wanaweza kushirikiana na sisi kama wadhamini kweye project hii ya GSS bado milango ipo wazi na tutafurahi sana kushirikiana na ninyi katika project GSS 2016 ,Uwanja wetu ni mpana na jukwaa letu ni kubwa hivyo itakua ni nafasi ya manufaa kwetu na kwenu pia kama mtaamua kutuunga mkono nkwa udhamibni katika project hii ya GSS 2016 kwa hatua zilizosalia za nusu fainali na fainali. Baada ya kusema haya ninaomba niwashukuru tena kwa uwepo wenu na hayo ndio yalikua maelezo juu ya lile lililotuweka hapa siku ya leo.

KANDANDA DAY 2016 KUCHANGISHA MADAWATI

Posted: 05 Sep 2016 09:06 AM PDT

TAMASHA la Kandanda maarufu kama ‘Kandanda Day’, linatarajia kufanyika Oktoba 15,  mwaka huu katika kiwanja cha Jakaya Kikwete Park (zamani Kidongo Chekundu).

Katika tamasha la mwaka huu,kauli mbiu itakuwa ni ‘Mpira na Dawati’ ikiwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kununua madawati yatakayogawiwa kwa shule mbalimbali nchini.

Mratibu wa tamasha hilo,Mohamed Mkangara,amesema kwamba mwaka huu wameamua kuja na kauli mbiu hiyo, ili kuunga mkono kampeni inayoendelea ya Serikali kuhusu madawati kwa shule za msingi na sekondari.
 “Umekuwa ni utaratibu wetu kila mwaka huu,kuja na kauli mbiu ambayo itahusisha soka na jambo ambalo moja kwa moja linaihusu jamii,kwahiyo, tumeona kwa kutumia soka,tunaweza kuisaidia jamii yetu kwa urahisi,”amesema  Mkangara

“Ndio maana kwa miaka yote tuliyofanya tamasha letu,kumekuwepo na ‘impact’ ya moja kwa moja kwa jamii inayotuzunguka,kwa hiyo ule utamaduni wetu tuliokuwa nao kwa miaka minne tunaendelea nao kwa mwaka huu kwa kukusanya fedha kwa ajili ya manunuzi ya madawati,ambapo tunatarajia kuchangisha fedha na kuuza jezi katika ‘dinner’ maalum ambayo tumeandaa kwa wadau mbalimbali.”
Mkangara,amesema kwamba madawati ambayo yatapatikana yatagawiwa kwa wawakilishi waliochaguliwa wa Kandanda kutoka mikoa mbalimbali nchini, ambao watahudhuria siku hiyo.

Tamasha la mwaka huu linatarajia kushirikisha timu mbalimbali alikwa,ukiacha timu wenyeji Time Dizo Moja na Timu Ismail.Pia,tamasha hilo linatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali na michezo ya kuvuta kamba kwa washiriki.

MBEYA CITY WARUDI NYUMBANI KUWAWINDA AZAM FC

Posted: 05 Sep 2016 08:37 AM PDT

BAADA ya safari ndefu katika mikoa ya kanda ya ziwa, kikosi cha Mbeya City Fc tayari kimewasili jijini Mbeya kujiwinda na mchezo ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Azam Fc uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Sokoine.

Muda mfupi  uliopita meneja wa kikosi hiki Geoffrey Katepa amesema kuwa Mwalimu Kinnah Phiri ameamua kuwapa mapumziko ya siku moja wachezaji wake ili waweze kupumzika kutokana na uchovu wa safari ndefu na siku ya kesho jioni wataingia  kwenye uwanja wa Sokoine  kuanza mazoezi ya matayarisho ya mchezo huo wa jumamosi.

“Mwalimu ametoa mapumziko siku ya leo hii ni kwa sababu tumekuwa na safari ndefu kutoka Mwanza tukipitia Tabora, hivyo mazoezi ya matayarisho ya mchezo ujao yataanza kesho jioni, jambo muhimu ni kwamba tunamshukuru Mungu  kwa kutuwezesha kupata matokeo mazuri kwenye michezo yetu mitatu ya mwanzo wa msimu,hili limetufanya kuongoza ligi kwa mara ya kwanza, jambo ambalo pia limetuongezea morali kubwa ya kushinda dhidi ya Azam Fc jumamosi” alisema.

Akiendelea  zaidi Meneja Katepa alisema kuwa kitengo cha utabibu cha City kinachoongozwa na Dr Joshua Kaseko  kimesibitisha kuwa  wachezaji wote wako kwenye hali nzuri kwa maana ya hakuna aliye majeruhi  na baada ya mapumziko ya leo wote watakuwa tayari kwa mazoezi ya kujiandaa kucheza mchezo wa jumamosi.

“Jopo la madaktari wetu wamenithibitishia kuwa kikosini  hakuna mchezaji mwenye majeraha, wote wana hali nzuri  hivyo baada ya kupisha mapumziko ya leo wote watakuwa tayari kwa mazoezi ya matayarisho ya mchezo”. alimaliza.

Kwenye michezo mitatu iliyopita  City  ilifanikuwa kuibuka na pointi  7, kufuatia suluhu ya bila kufungana na Kagera Sugar na baadae kuiadhibu Toto Africans bao 1-0 na mwisho kuhitimisha kwa kuifunga Mbao Fc  bao 4-1 na kushika  usukuni wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

TTCL YATOA HUDUMA YA INTANETI BURE MKUTANO WA WANASAYANSI DAR.

Posted: 05 Sep 2016 08:01 AM PDT

 Mmoja wa maofisa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL (kushoto) akimwelezea mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa sayansi nchini 'The 3rd Sci-GaIA thematic Workshop' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Teknonolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na European Commission. TTCL imetoa huduma ya intaneti bure kwa wadau wa mkutano huo na kufanya maonesho ya bidhaa na huduma zake mpya mbalimbali.  Timu ya mauzo ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ikiwa katika banda lao nje ya mkutano wa Tatu wa wadau wa sayansi nchini 'The 3rd Sci-GaIA thematic Workshop' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Teknonolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na European Commission. TTCL imetoa huduma ya intaneti bure kwa wadau wa mkutano huo na kufanya maonesho ya bidhaa na huduma zake mpya mbalimbali. Baadhi ya washiriki wa mkutano wa tatu wa wadau wa sayansi nchini 'The 3rd Sci-GaIA thematic Workshop' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, ulioandaliwa na Taasisi ya Teknonolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na European Commission wakishiriki katika mkutano huo. TTCL imetoa huduma ya intaneti bure kwa wadau wa mkutano huo na kufanya maonesho ya bidhaa na huduma zake mpya mbalimbali. Baadhi ya washiriki wa mkutano wa tatu wa wadau wa sayansi nchini 'The 3rd Sci-GaIA thematic Workshop' ulioandaliwa na Taasisi ya Teknonolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na European Commission wakiwa katika banda la maonesho ya bidhaa mpya za TTCL wakipokea vipeperushi vya kampuni ya TTCL vinavyoelezea bidhaa na huduma zao mpya.
                                            KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

SIKUKUU YA EID YA KUCHINJA KUADHIMISHWA KITAIFA JIJINI DAR

Posted: 05 Sep 2016 02:25 PM PDT


NEWZ ALERT:Naibu waziri Tamisemi,Selmani Jafo anusurika kifo ajalini Mbeya

Posted: 05 Sep 2016 07:28 AM PDT


Gari la Naibu Waziri wa Tamisemi likionekana baada ya kugongwa katika ajali hiyo.

Gari lililoigonga gari la Naibu Waziri likiwa limetupwa korongoni.

Askari wa usalama barabaran wilaya Rungwe, Mbeya wakipima ajali ilivyotokea.


Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amepata ajali eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.

Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ta Corola iliyokuwa ikotokea Mbeya kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu kikazi.

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema katika gari Waziri walikuwa watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva na wote walitoka salama katila ajali hiyo.

Alisema baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo walifanya uchunguzi kama wameumia kwa ndan au laa! Lakin bahat nzuri Daktari aliyewafanyia uchunguz alisema hakuumia popote ni wazima.

Alisema baada ya hapo Waziri na watu waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge
 

Picha zote kwa hisani ya Mbeya yetu

POLISI KANDA MAALUM DAR WAVUNJA MTANDAO WA MAJAMBAZI.

Posted: 05 Sep 2016 06:55 AM PDT

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  limefakiwa kukamata watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi hatari  ambao wamekuwa wakishiriki matukio mbalimbali ya uhalifu kwa kutumia silaha.

Watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi walipatikana na bunduki 23 za aina tofauti tofauti, Risasi 835, kifaa cha kuzuia risasi kuingia mwilini tatu (Burret Proof), Sare za Polisi, Pingu 48 pamoja na Radio 12 za mawasiliano.

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya kanda  maalum, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amesema kuwa majambazi hao walikuwa na mtandao mkubwa ikiwa ni kununua silaha nje ya nchi  kwa ajili ya kufanyia uhalifu katika maeneo mbalimbali.

Kamanda Sirro amesema baada ya tukio hilo timu ya polisi ya upelelezi  iliweka mtego na kufanikiwa kukamata majambazi watatu maeneo ya Mbagala, Keko na Kawe.

Kamanda Sirro amesema katika mahojiano walikiri kufanya tukio katika benki ya Habib African maeneo ya Kariakoo 2014 na Stanbic 2014.

Amesema kuwa majambazi walikiri kuwa na wenzao wako katika msitu wa Vikindu.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha kifaa cha kuangalia wakati wakifanya uhalifu majambazi kwa waandishishi wa habari ikiwa ni sehemu ya vifaa vilivyokuwa vikitumika na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha bunduki  kwa waandishi wa habari ikiwa ni sehemu yabunduki zilivyokuwa zikitumika na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya operesheni walioifanya na kukamata majambazi watatu katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.
Kusoma zaidi bofya HAPA.

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA KAMATI YA MAZINGIRA NA KILIMO YA BUNGE LA SWEDEN.

Posted: 05 Sep 2016 06:28 AM PDT

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba akiongea na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt. Balozi huyo aliambatana na Kamati ya Mazingira na Kilimo ya   Bunge la Sweden.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba (Kulia) akifurahia jambo na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Mazingira na Kilimo kutoka  Sweden walipomtembelea Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli Jjijni Dar es Salaam leo.
Sehemu ya wabunge kutoka Sweden wakifuatilia mazungumzo baina ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba. Ujumbe huo wa Wabunge ulimtembelea Mh. Waziri na kujadili masuala ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

BARAZA LA MADIWANI ILALA LAUNGANA KUIPIGA TAFU ASHANTI UNITED.

Posted: 05 Sep 2016 07:50 AM PDT

  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akizungumza wakati wa hafla iliyowakutanisha Baraza la Madiwani na Uongozi wa Ashanti United iliyofanyika mwishoni mwa wiki na kuisaidia timu hiyo kurejea ligi na itakuwa chini ya Manispaa ya Ilala                      
 Kulia ni Diwani wa kata ya Ilala, Saadi Khimji na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Ashanti United Almas Kasongo.
 Makamu Mwenyekiti wa Ashanti United United Almas Kasongo akizungumza na kueleza changamoto walizokuwa nazo katika kuendesha timu na kumshukuru Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko(kulia) kwa hatua nzuri waliyoifikia ya kuamua kuisaidia timu yao.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kayeko akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa timu ya Ashanti jijini Dar es Salaam.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko ameitaka klabu ya Ashanti kuhakikisha wanarejea ligi kuu kwani kwa sasa wapo nao bega kwa bega.

Hatua hiyo imekuja baada ya Manispaa ya Wilaya ya Ilala kuona umuhimu wa kuwa na timu na sasa Ashanti itakuwa chini ya Manispaa na wataisimamia kwa hali na mali.

Akizungumza na Viongozi wa Ashanti pamoja na Baraza la Madiwani,  .Charles Kuyeko amesema Ashanti ni timu kubwa kwani ina muda mrefu sana na imeweza kuhimili kujiendesha kwa fedha chache za wanachama na zimekuwa hazitoshelezi kulingana na bajeti yao ya kila mwaka.

Kuyeko amesema kuwa kuna timu nyingi sana zinazosimamiwa na Manispaa na zimekuwa zikifa ya vizuri na zaidi ukiangalia kwa timu za Ilala zinazoshiriki  ligi daraja la Kwanza ukiacha Simba na Yanga zilizowafuata kuhitaji msaada wao zaidi ya Ashanti na baraza zima la madiwani wameahidi kushirikiana nao kwa hali na mali.

Kwa niaba ya uongozi wa Ashanti United, Makamu Mwenyekiti Almas Kasongo amesema kuwa wamepokea taarifa hiyo kwa bashasha kubwa sana hasa ukifikiria walikuwa na upungufu wa bajeti ya 2016/2017 ya takribani milioni 75, na zaidi ukiachilia hilo uwepo wa Baraza la Madiwani katika timu yao ya Ashanti utaleta hamasa kubwa sana kwa watu wengine kujitokeza kuja kuisaidia.

Ashanti United imeweza kuwakutanisha baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilala takribani 30 na wote wameonyesha nia ya kuiunga mkono timu hiyo na kwa kuanzia kwenye hafla hiyo, Mstahiki Meya alitangaza kuanza na Milioni tano lakini watakapokutana tena watasema ni kiasi gani watakitoa na watakapokuwa na shida wasisite kupiga hodi kwake.

WATOA TAARIFA ZA UHALIFU NA MASHAHIDI KUANZA KULINDWA

Posted: 05 Sep 2016 05:44 AM PDT

Mkurugenzi Msaidizi Utekelezaji wa Katiba kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Kamana Stanley akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kuanza kutekelezwa kwa Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi ya mwaka 2016 inayolenga kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya uhalifu nchini. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa wizara hiyo Sheiba Bullu.


Na. Fatma Salum – Dar es salaam.

Serikali imeanza kutekeleza Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi ya mwaka 2016 (The Whistleblower and Witness Protection Act. 2016) ili kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya uhalifu nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Msaidizi Utekelezaji wa Katiba kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Kamana Stanley wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kuanza kutumika kwa sheria hiyo.

Stanley amesema kuwa  kuwepo kwa sheria hiyo kutasaidia kuwapatia ulinzi wa kisheria wale wote wanaotoa taarifa za uhalifu wa makosa ya aina mbalimbali wanayoshuhudia yakitendeka. Vilevile itarahisisha utoaji na upatikanaji wa taarifa za uhalifu kwani sasa taarifa hizo zitatolewa na kupokelewa sio tu kwenye vyombo vya dola pekee bali pia kupitia vyombo vya habari na vyanzo vingine vinavyobainishwa katika sheria hiyo.

“Wananchi wasiwe na woga kujitokeza kutoa taarifa za uhalifu na matendo ya aina zote yanayofanywa kinyume cha sheria kwani taarifa hizo zitakuwa siri na zitafanyiwa kazi bila ya kuwataja watoa taarifa. Pia mashahidi wanapotakiwa kufika mahakamani wasiogope kwani sheria hii inawalinda” amesema Stanley. 

Amefafanua kuwa wahusika watakaoshindwa kushughulikia vyema taarifa zinazotolewa kwao na kuruhusu watoa taarifa na mashahidi kupata madhara, sheria hiyo imeweka utaratibu wa namna ya kushughulika nao.

Aidha, Stanley ameeleza kuwa katika sheria hiyo wale ambao taarifa zao zitafanikisha kuokoa mali ya umma, kupatikana kwa wahalifu na kulinda mazingira na maisha ya binadamu kutokana na uhalifu uliopangwa kufanyika, wamewekewa utaratibu wa kupatiwa motisha ikiwa ni pamoja na kuwafidia wale ambao wataathirika kutokana na taarifa walizotoa.

Stanley ameongeza kuwa Serikali inatarajia kwamba kutungwa kwa sheria hii kutaleta matokeo chanya katika kupambana na uhalifu wa aina zote hivyo kukuza ari ya wananchi kusimamia wenyewe juhudi za kujiletea maendeleo.

“Masuala ya usimamizi wa utawala wa sheria yataimarika kutokana na kuwepo kwa utayari wa wananchi kushiriki katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kufika katika vyombo vya sheria kutoa ushahidi. Pia ushiriki wao katika kufichua maovu yakiwemo yanayosababisha hasara kwa taifa utasaidia kuinua uchumi ukizingatia kwamba sasahivi Serikali inapambana sana na mafisadi” ameeleza Stanley.

Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi ya mwaka 2016 (The Whistleblower and Witness Protection Act. 2016)imeanza rasmi kutumika Julai Mosi mwaka huu baada ya kuidhinishwa na Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.

TAARIFA YA AJALI YA BASI LA HOOD LIKITOKEA MBEYA KWENDA ARUSHA

Posted: 05 Sep 2016 05:21 AM PDTLINDI, ARUSHA KUFUNGUA DIMBA AIRTEL RISING STARS TAIFA.

Posted: 05 Sep 2016 05:48 AM PDT

 Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde akiongea wakati wa kuchezesha droo ya fainali za taifa ya michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars. Kushoto ni Mkurungenzi wa maendeleo ya soka la wanawake TFF Amina Karuma na katikati Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi. Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi.
 Mkurungenzi wa maendeleo ya soka la wanawake Tanzania Amina Karuma akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa. Katikati ni Mkurungenzi wa Ufundi TFF na kulia Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jana Matinde.
Mkurungenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa. Kushoto ni Mkurungenzi wa maendeleo ya soka la wanawake Tanzania Amina Karuma.

TIMU za soka za wasichana za Lindi na Arusha zimepangwa kukutana katika mechi ya fungua dimba ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Statrs ngazi ya taifa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam, Jumanne, Septemba 6, 2016.

Mashindano hayo yanayojumuisha timu za wasichana na wavulana yatafunguliwa rasmi siku hiyo ya Jumanne mchana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ambaye atashuhudia mechi ngumu ya wavulana kati ya Mwanza na Ilala.

Timu nyingine zinazoshiriki katika michuano hiyo yenye lengo la kuibua vipaji ni Temeke, Kinondoni, Morogoro, Arusha, Mbeya, Lindi na Zanzibar. Tayari timu zimeshawasili na kupiga kambi katika shule ya Filbert Bayi iliyoko Kibaha.

Akizungumza wakati wa hafla ya kupanga makundi iliyofanyika katika ofisi za shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), Mkurungenzi wa Ufundi Mwalimu Salum Madadi alisema kuwa maandalizi yote ya mashindano hayo ngazi ya taifa yamekamilika.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na mkurengenzi wa maendeleo ya soka la wanawake nchini Bi Amina Karuma ambaye aliyaelezea mashindano ya Airtel Rising Stars kuwa ni chemchem ya wanasoka chipukizi wasichana kwa wavulana.

“Mashindano ya Airtel Rising Stars yametusaidia kupata wachezaji wenye vipaji vya ajabu ambao wanaunda timu za Serengeti Boys na timu ya taifa ya wanawake yaani Twiga Stars”, alisema na kuwashukuru Airtel Tanzania kwa kuendelea kudhamini mashindano hayo.

Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde alisema kuwa kampuni yake inajivunia kuweza kutoa mchango katika soka la Tanzania. “Airtel Rising Stars imekuwa chanzo cha kutumainiwa kwa klabu na timu za Taifa kupata vijana chipukizi wenye vipaji. Tunaona fahari kuweza kupata fursa ya kudhamini soka nchini Tanzania“alisema Matinde.

Michuano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa inatarajia kufikia tamati siku ya Jumapili, Septemba 11, 2016 ambapo bingwa kwa upande wa wasichana na wavulana watapatikana na kukanidhiwa vikombe vya ubingwa.

Vilevile TFF itatangaza wachezaji nyota kwa wasichana na wavulana wataochaguliwa kuunda timu ya Airtel Rising Stars mwaka 2016.

ZANTEL WAZINDUA OFA YA JIBWAGE NA MBUZI KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA IDD.

Posted: 05 Sep 2016 05:37 AM PDT

 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua ofa maalumu kwa wateja wanaotumia mtandao wa simu za Mkononi wa Zantel ofa ya shinda mbuzi, pamoja na kutoa mbuzi kwa Vituo 50 vya kulelea watoto yatima jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi Mbuzi mwakilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Kurasini National Childrens Home, Silas Kusewa Kurasini jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi Mbuzi mwakilishi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Tanzania Mitindo House Klichopo Kiamboni, Khadija Mwanamboka mara baada ya Mkurugenzi huyo kuzindua Ofa maalumu kwa wateja wake ya shinda mbuzi.

KAMPUNI ya Simu za Mkononi Zantel imezindua Kampeni ya Jibwage na Mbuzi katika kusherehekea Sikukuu ya Idd el Adha, ikitambulika pia kama 'Sherehe ya Kuchinja' kwa kutoa mbuzi 500 kwa wateja wake wenye matumizi ya  zaidi huku mbuzi 100 wakigawiwa katika vituo mbalimbali vya watoto yatima nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin amesema "Hii ni sehemu ya kuwashukuru wateja wetu na kusherehekea pamoja nao Sikukuu ya Idd. Imekuwa ni utamaduni wetu kurudisha katika jamii kupitia kampeni na miradi mbalimbali, hivyo kwa leo Zantel inatoa mbuzi 500 katika kusherehekea Sikukuu hii ya Kuchinja.”

Idd el –Adha ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha kwa kuonyesha umuhimu wa kutoa sadaka kwa kuchinja na ibada.

Mbuzi 400 watatolewa kwa wateja wa Zantel wenye matumizi zaidi kuliko wengine na ambao watakuwa wamejisajili katika kampeni kwa kupitia *149*15# na kuchagua  “Jibwage na Mbuzi”. Kujisajili katika promosheni hii ni bure kwa wateja wote wa Zantel. Kila siku wateja 40 watakaokuwa wametumia muda zaidi watajizawadia mbuzi.

 “Hii si bahati nasibu, wale wateja wa juu watakaokuwa wametumia dakika nyingi bila kuchezeshwa mchezo wa bahati watakuwa wamejizawadia moja kwa moja hivyo natumia fursa hii kuwahamasisha wateja wetu kujisajili ili kupata mbuzi na kusambaza furaha ya Eid katika familia zao” alisema  Benoit

Mbuzi 100 wanaobaki watatolewa msaada kwa  vituo vya watoto yatima vilivyochaguliwa katika mikoa mbalimbali. 

“ Pia tunatumia nafasi hiyo hiyo kusaidia watoto yatima na wale wasioweza kufanikisha sadaka hii ya kuchinja ili nao wafurahi pamoja na wengine na kushiriki upendo unaotokana na Idd”,  ameongeza.

Miongoni mwa miradi ambayo Zantel imetoa misaada ni mradi wa kina mama wanaozalisha zao la mwani Unguja, huduma za maktaba Zanzibar –Zanzibar Library Services, vile vile kompyuta na internet ya bure kwa kikundi cha wasanii cha Mkubwa na Wanawe na vituo mbali mbali vya walimu Zanzibar.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

SONGAS FOOTBALL CLUB WAENDESHA BONANZA LA KUHAMASISHA MICHEZO.

Posted: 05 Sep 2016 05:09 AM PDT


Mgeni Rasmi katika Bonanza hilo Albert Kimaro ambaye ni Mkufunzi Mwandamizi Idara ya Michezo Chuo Kikuu cha Dar es salaam akikagua moja ya Timu hizo katika Bonanza hilo.
Moja ya timu ikiwa imefungwa goli la kizembe huku goli kipa asijue cha kufanya na wachezaji wengine kukimbia kwa ajili ya kujipanga zaidi.
Mpira ukiendelea huku watu mbalimbali wakifuatilia Burudani hiyo kwa makini.
Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa.

MAMA BISHANGA NA WADOGO ZAKE WAFIWA NA MAMA YAO MWALIMU AGNES NDEMBO HATIA

Posted: 05 Sep 2016 03:15 AM PDT

 Mama Hatia na wanae, wajukuu na vitukuu
 Watoto wa marehemu mzee Isaya Innocent Hatia tumempoteza mpendwa mama yetu mpendwa Mwalimu Agnes Ndembo Hatia kilichotokea hospitali ya Regency  jana jumamamosi mchana. Mama yetu alikuwa nguzo pekee iliobakia nasi baada ya kufariki baba yetu Mzee Isaya Innocent Hatia mwaka 2011. Tunamshukuru Mungu sana kwa upendo wake kwa mama yetu aliempa nguvu ya kuishi miaka tisini na sasa amempenda zaid mama yetu, bibi yetu na amempumzisha usingizi 

wa milele na milele Ameni

Mwalimu Agnes Ndembo Hatia amefundisha watu wengi sana darasa la kwanza
tangia miaka ya hamsini hadi alipostaafu Tabora, Uhuru shule yamsingi.
Mama, ametuacha watoto wake Christina wa USA, Geofrey wa Namibia, Mwl Mark Hatia wa Tambaza shule ya secondary, Bernadetta wa Dar, Isaya wa Finland, Costancia wa Kibaha, na Oscar mdogo wetu wa mwisho. Ameacha wajukuu, na vitukuu wengi ambao ni watoto na wajukuu zetu sisi watoto wake pamoja na dada
zetu marehemu Joyce Hatia na Mwalimu Cecilia Hatia. 
Picha zinaonyesha mama Hatia mwaka 1966 akiwa na Constacia ambae picha yake pembeni ni Costancia alivyo sasa, na zingine ni
Kwa taarifa za maandalizi na ratiba piga simu zifuatazo. 0653 763 201 Kilian Kamota,
0755 333 948 Dick Hatia, 0788 627 430 Ibra Yunus, na 0763 833 893 Solmon.
 BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA. TUMSIFU YESU KRISTO: AMENMama Hatia mwaka 1966 akiwa na Constacia ambae picha yake pembeni ni Costancia
alivyo sasa,

MUSWADA WA HUDUMA ZA VYOMBO VYA HABARI KUSOMWA BUNGENI KWA MARA YA KWANZA.

Posted: 05 Sep 2016 03:33 AM PDT

Anitha Jonas – WHUSM.
MUSWADA wa Huduma za Vyombo vya Habari  kusomwa kwa mara ya kwanza Bungeni  Septemba hii na  kujadiliwa  Desemba Mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na  TBC 1,chenye lengo la Mawaziri kueleza umma namna wanavyotekeleza majukumu.

“Muswada huu mzuri na utasaida kuleta suluhishi la malalamiko ya kuwepo kwa sheria kandamizi,pia itasaidia kukuza tansia ya habari pamoja na kuifanya tasnia ya habari kuheshimiwa kama tansia nyingine”,alisema Waziri Nnauye.

Waziri Nnauye alisisitiza kuwa uandaaji wa Muswada  ulishirikisha wadau mbalimbali na kuzingatia maoni yao na serikali itaendelea kupokea maoni ya wadau  hata mara baada ya kusomwa kwake.
Pamoja na hayo Waziri huyo mwenye dhamana na sekta ya habari nchini  kupitishwa kwa Muswada huo kutasaidia kutoa suluhisho la kuwepo na changamoto katika sekta ya utangazaji ambayo kwa sasa inaonekana kupoteza mulekeo.

Aidha,Waziri Nnauye alisema kuwa serikali inataka kuipeleka  tansia  ya habari mbali  na kupitia Muswada huo utasaidia kufanikisha hilo kwani umeeleza kuwa mwandishi anahitajika kuwa na digrii na hii ni kwalengo la kuweka heshima ya taaluma kama ilivyokwa taaluma nyingine mfano sheria.
Halikadhalika Waziri huyo alizungumzia kuwepo na changamoto  katika Sheria ya Utangazaji kwani imekuwa haionyeshi  Mtangazaji anaporusha kipindi hewani kilicho kinyume na maadili ni adhabu gani apewe.

“Tungependa sheria ijayo iweze kumbana mwandishi pale anapokosa maadili na kumchukulia hatua kama ilivyo kwa tansia nyingine kama uhandisi na sheria kufikia hatua kufutiwa utoaji wa huduma hiyo”,alisisitiza Mhe.Nnauye.

Akizungumza  kuhusu changamoto ya upatikanaji  wa taarifa kutoka kwa wasemaji wa taasisi za Serikali Waziri Nape alisema tayari ametoa agizo kwa watendaji kuwashirikisha wasemaji katika vikao vya maamuzi ili waweze kuwa na taarifa za pamoja na kuwapa nafasi ya kusema ikiwa na sehemu ya kazi yao.

Hata hivyo Mheshimiwa Waziri ameliahidi Shirika la Utangazaji nchi kulisaidia kutatua changamoto zinazolikabili ikiwemo uhaba wa vifaa,pamoja na kuboresha maslai ya watumishi wake.Pia ameeleza  Bodi mpya ya TBC 1 iliyoundwa  imepitia  mkataba wa TBC 1 na STARTIMES  kwa lengo la kutaka kuiboreshea mazingira shirika hilo na tayari imekwisha maliza kazi na kuwasilisha mapendekezo.

MAADHIMISHO YA MIAKA 18 YA HOME GYM YAFANA.

Posted: 05 Sep 2016 03:04 AM PDT

 Walimu wa Home Gym wakikata keki ya maadhimisho ya miaka 18 kwa pamoja katika sherehe zilizofanyika fukwe za Escape One mwishoni mwa wiki.
 Keki maalum
Wanachama wa Home Gym Wakiwa katika mazoezi mbalimbali

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MKURUGENZI wa Kituo cha kufanyia mazoezi ya viungo Home Gym, Andrew Mangomango amesema kuwa kwa mwaka huu maadhimisho ya miaka 18 toka kuanzishwa kwake yatazunguka katika baadhi ya mikoa.

Akizungumza wakati wa maadhimishi hayo yaliyifanyika Katika fukwe za Escape One mwishoni mwa wiki, Mangomango amesema kuwa ndani ya miaka 18 ameweza kupata wanachama wa kudumu takribani 200 na ameweza kuwasaidia watu mbalimbali kufahamu jinsi gani ya kufanya mazoezi.

Mangomango amesema kuwa, maadhimisho haya ni ya tano mfululizo na kwa mwaka wameamua kutembelea baadhi ya mikoa ikiwemo Tanga, Arusha na Mwanza ambapo baadhi ya wanachama wake wa siku nyingi wapo kule na watatumia fursa hiyo kuhamasisha watu mbalimbali kufanya mazoezi kwa afya.

"Na katika kuendeleza michezo, Kituo cha Home Gym kimeweza kutoa walimu takribani nane ambao wote wameshafungua Gym zao mikoa mbalimbali, hii ni moja ya mafanikio tuliyoyapata na zaidi bado tunashirikiana nao na hata leo kwenye maadhimisho haya wapo wote wamekuja kuunga mkono jitihada za Home Gym,"amesema Mangomango.

Katika maadhimisho yaliyohudhuriwa na baadhi ya wadau wa michezo ikiwemo Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG, Imani Kajura, waandishi wa habari mbalimbali na taasisi zingine wameonyesha muitikio mkubwa wa kufanya mazoezi na kuhamasisha watu wajitokeze kwani Michezo ni Afya.

Kwa mwaka huu, Mangomango amesema kuwa mwaka huu watafanya maadhimisho yao sambamba na Kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14, mkoani Arusha.

DKT INTERNATIONAL TANZANIA YAZINDUA ‘TRUST COMMUNITY MATERNITY HOMES

Posted: 05 Sep 2016 03:21 AM PDT

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la DKT International Tanzania Raphael da Silva akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kliniki mpya za Shirika hilo zijulikanazo kama “Trust community maternity homes”. Kliniki hizo mpya ni maalumu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam.
Meneja Masoko wa DKT International Tanzania Sialouise Shayo akionyesha baadhi ya bidhaa kwa waandishi wa habari zinazopatikana kwenye Kliniki mpya ya uzazi wa Mpango iliyozinduliwa jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam. Kliniki hiyo ni maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango.
 Mkunga kutoka DKT International Tanzania Adella Hugo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Kliniki mpya ya uzazi wa Mpango iliyozinduliwa jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam. Kliniki hiyo ni maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango. 


SHIRIKA lisilo la kiserikali la DKT International Tanzania limezindua mfano wa Kliniki mpya ziitwazo “Trust community maternity homes kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kawaida zinazoendeshwa na wakunga mbalimbali.

“Trust Community Maternity Homes” – Ni kliniki zinazojitosheleza zilizotengenezwa kwa ubunifu kwa kutumia kontena ya kusafirishia mizigo, kliniki hizi zimetengenezwa maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu.

Kiliniki za “Trust Community Maternity Homes”  zilizinduliwa kwa umma  wakati wa uzinduzi wa kliniki ya “Trust Health & Wellness Clinic “ ya Dar Es Salaam na ofisi  mpya za DKT International Tanzania  mnamo tarehe mbili September, 2016

“Kila mwaka, wanawake milioni moja hapa Tanzania ambao hawakukusudia kupata ujauzito hupata ujauzito” alisema mkurugenzi mkuu wa DKT international, Raphael da Silva.

“Hali hii si tu kuwa ina athiri wanawake hawa kifedha, afya zao binafsi na hali ya kiuchumi ya familia zao, lakini pia zinapelekea kuongeza uhitaji wa Serikali kutoa huduma za kiafya pamoja na elimu kwa watoto hawa .Kama tunaweza kufanikisha kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu za afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa jamii katika miji midogo na wanajamii ambao hawapati huduma hizi kiurahisi, tutafanikiwa kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wanawake hawa” alisema.

“Trust Community Maternity Homes ni kliniki zinazojitosheleza ndani ya kontena la kusafirishia mizigo, zinazoendeshwa na wakunga wataalamu na wenye uzoefu wa muda mrefu kama washirika chini ya kliniki mama za “Trust health and wellness clinics” .  Alisema meneja mradi, Karoli Mango.

“Kliniki hizi zinatoa ubora ule ule wa huduma , usiri na msaada  sawa sawa na Kliniki zetu nyingine za Trust  zinazopatikana mikoani hapa nchini .Kliniki yetu ya kwanza ya “ Trust community maternity homes” ya mjini  Kahama iko katika hatua za mwisho za  maandalizi kabla ya ufunguzi” aliongeza.

Trust ina mpango wa kuingia mikataba yenye masharti mepesi na wakunga wazoefu ambayo itawawezesha kukodisha na baadae kuzi miliki kliniki hizi.  Wakunga wanaotoa huduma hizi watatumia kliniki hizi ambazo ziko ndani ya kontena ambazo zinatumia umeme wa sola , zenye uwezo wa kutoa huduma kamili za afya ya uzazi na uzazi wa mpango, pamoja na huduma nyingine za afya kwa jamii. Wakunga hawa watajipatia kipato kwa kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa huduma na bidhaa zitakazo tolewa katika kliniki hizi. 

Kwa sasa , kuna “ Trust health and wellness  clinic” nne  ambazo ziko Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya and Mwanza  na pia kuna kliniki  na hospitali washirika  30  ambazo zinatoa huduma kwa kutumia chapa ya Trust. 

Kliniki ya Msasani peninsula ya Dar Es Salaam ilifunguliwa mapema mwezi Julai.

Mkutano wa wadau kujadili Mpango Kazi wa Taifa kuhusu Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP III)

Posted: 05 Sep 2016 02:32 AM PDT


6.97Score
Be the first to
mark Beautiful

Email Newsletter

Sign up for our email newsletters

Facebook Page

Twitter Page

Recent Post

Tags