|
|
MICHUZI BLOG

MICHUZI


Chuo cha Uhasibu Arusha kinakaribisha maombi ya kujiunga na chuo hicho kwa muhula mpya katika ngazi mbalimbali

Posted: 09 Jul 2017 01:05 PM PDT

Chuo cha Uhasibu Arusha kinakaribisha maombi ya kujiunga na chuo hicho katika ngazi za Cheti, Diploma, Bachelor, Postgraduate diploma na Masters katika fani zifuatazo:

- Accountancy

- Finance and Banking

- Business Management

- Economics and Finance

-Computer Science na
- Information Technology
Chuo kina kampasi Arusha, Dar es salaam,
Mwanza na Babati mkoani Manyara.

Watumishi wa IAA katika banda lao viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Nyerere (SABASABA) barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam wakiwa tayari kukuhudimia. Banda lao lipo jengo la Wizara ya Fedha na mipango.

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AWASILI CHATO KWA AJILI YA KUKABIDHI NYUMBA 50 ZA WATUMISHI WA AFYA KATIKA MIKOA YA SIMIYU, KAGERA NA GEITA

Posted: 09 Jul 2017 11:31 AM PDT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Chato mkoani Geita. Rais Mstaafu Mkapa katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya (Mkapa Foundation) katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita. Kushoto ni Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita. Balozi huyo wa Japan katika siku ya kesho anatarajiwa kukabidhi mtambo wa kukamua Mafuta ya Alizeti (Double Refine) uliojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali ya Japan.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa nyumbani kwake Chato mkoani Geita
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa pamoja na wageni mbalimbali waliofika Chato kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazotarajiwa kufanyika kesho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Geita Josheph Kasheku Msukuma aliyefika Chato pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita. 
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

SAFARI YA MWISHO YA MAREHEMU HASSAN RASHID SHEBUGE, ALIYEKUWA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI

Posted: 09 Jul 2017 10:44 AM PDT

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Jumamosi Julai 6, 2017 ameongoza waombolezaji wakiwemo ndugu, jamaa, marafiki, majirani na wafanyakazi wenzie katika mazishi ya aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyefariki dunia siku ya Alhamisi, Julai 6, 2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupatwa na shinikizo la damu.
Marehemu Shebuge, aliyeagwa siku ya Ijumaa Julai 7, 2017 nyumbani kwake Mbagala Majimatitu Jijini Dar es Salaam amezikwa Jumamosi Julai 8, 2017 katika kijiji cha Funta, Bumbuli, mkoani Tanga.
 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Rashid Shebuge likiwasili kwenye eneo la makaburi  la kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella na waombolezaji wengine wakiwa kwenye mazishi ya aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella  akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
Ndugu wa marehemu  akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.
Msaidizi wa Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Kaganda akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya  aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid Shebuge makaburi  ya kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga. Kupata habari zaidi BOFYA HAPA

WAZAZI WASHAURIWA KUTUMIA AKAUNTI YA MTOTO NA CHIPUKIZI YA NMB

Posted: 09 Jul 2017 01:35 PM PDT

BENKI ya NMB imewashauri wazazi na walezi kuwafungulia watoto wao akaunti mbili mpya ambazo zimeanzishwa na benki hiyo ya Mtoto Akaunti na Chipukizi Akaunti kwa ajili ya kutumia kuwawekea fedha watoto wao.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Elimu ya Fedha wa benki ya NMB, Ryoba Mkono baada ya kutoa elimu ya fedha kwa wazazi na watoto kwenye maonesho ya 41 ya Saba Saba yanayofanyika jijini  Dar es Salaam. Mkono alisema mzazi atakuwa na nafasi ya kuchagua akaunti gani inamfaa mtoto kulingana na umri wake na kwa kila akaunti mtoto atakuwa anapata riba ya asilimia tano kila mwisho wa mwaka kulingana na kiasi cha fedha alichonacho kwenye akaunti.

“Mtoto Akaunti inahusisha watoto wenye umri kuanzia miaka 0 hadi 17 gharama yake ya kufungua ni 5,000. Ni akaunti ya kuweka akiba na mzazi ndiyo anaweza kuweka na kutoa na mara nyingi tunashauri mzazi asitoe ili itumike kwa mtoto baadae.”

“Kwa upande wa NMB Chipukizi Akaunti hii inahusisha watoto wenye umri wa miaka 13 hadi 17 ni akaunti ambayo ina ATM Card na mtoto anaruhusiwa kutoa pesa hadi 50,000 kupitia ATM zetu au NMB Wakala kwa siku moja na kila akitoa pesa mzazi anapata ujumbe kuwa mtoto katoa pesa,” alisema Mkono.

Pia Mkono alizungumza kuhusu faida za akaunti hizo mbili tofauti na akaunti zingine ambazo zinapatikana kwenye benki ya NMB, ”Faida yake ni hazina makato ya mwezi kwa ajili ya uendeshaji, pia mtoto anapata riba ya asilimia tano ya kiasi alichonacho kwenye akaunti yake ya NMB.”

Aidha Mkono aliwashauri wazazi kuwafungulia watoto akaunti hizo ili wapate huduma boa kutoka NMB lakini pia hata katika kipindi cha maonesho ya Saba Saba watoto wataweza kutumia kadi zao kununua vitu mbalimbali ambavyo wanahitaji.

“Wazazi wamekuwa wakiwapa watoto pesa mkononi wanapoenda kwenye Saba Saba lakini kama mtoto ana miaka 13 anaweza kuwa na ATM Card ni vyema wakawafungulia akaunti ili wazoee kutumia pesa kwa uadilifu na hata mwakani wakija kwenye Saba Saba wanakuwa wanaweza kutumia kadi zao kutoa pesa ili kufanya matumizi yao,” alisema Mkono.

WAZIRI MKUU AWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAFANIKIO

Posted: 09 Jul 2017 09:26 AM PDT


*Asema nchi ina utulivu wa kisiasa na uchumi unaokuwa kwa kasi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji watakaokuja nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu wa kisiasa na uchumi wenye kukua kwa kasi.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 09, 2017) alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan alipochaguliwa kuwa Imamu Mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.

Ameupongeza mtandao wa taasisi za Aga Khan kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika kutoa kipaumbele cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.

“Nawahakikishia kwamba uwekezaji wenu hapa nchini utakuwa na baraka kwa sababu nchi imetulia kisiasa na uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee kuwaalika wanajumuia wa madhehebu ya Shia Ismailia popote walipo duniani waje kuwekeza nchini fursa bado zipo.”
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waiyo hudhuria katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waiyo hudhuria katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na mama Zakia Megji wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (kushoto) ni Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema Julai 9, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Muwakilishi wa AKD resident Amin Kurji katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli,(katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Aga Khan Suleiman Shabbudin Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

DKT. MPANGO ATEMBELEA BANDA LA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA, AKIPONGEZA KWA UTENDAJI WAKE

Posted: 09 Jul 2017 01:23 PM PDT


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango. (kushoto), akikaribishwa na Afisa Udahili wa Chuo Cha Uhasibu Arusha, (IAA), Bw. Gerald Malisa, alipofika kutembeela banda la chuo hicho lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasaba,barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanaendelea kwenye viwanja hivyo na yatafikia kilele Julai 13, baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kuomba Tan Trade waongeze siku tano zaidi ili kutoa fursa pana kwa wanachi kutembelea maonesho hayo na kupata faida mbalimbali.

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ametembelea banda la Chuo Cha Uhasibu Arusha, (IAA), lililoko kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kunakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.


Waziri alikipongeza chuo hicho kwa maendeleo kilichofikia na kusaidia kutoa wataalamu katika Nyanja za uhasibu na utunzaji wa hesabu ambapo sasa kinaendelea kupanua huduma zake kwenye maeneo mengine nje ya makao makuu yake jijini Arusha.Akimpatia maelzo waziri mpango, Afisa Uhusiano na Masoko wa chuo hicho, Sarah Goroi, alimueleza Waziri Mpango kuwa chuo hicho kwa sasa ukiacha makao makuu yake jijini Arusha pia kina matawi jijini Dar es Salaam, jijini Mwanza na wilayani Babati mkoa wa Manyara.


Sarah  alisema, chuo kinatoa elimu ya uhasibu ngazi ya Astashahada(certificate), Stashahada(Diploma), Shahada ya Kwanza(Bachelor degree), Post Graduate diploma, na Shahada ya Uzamili (Masters Degree).

“Mheshimiwa waziri huduma tunazozitoa kwenye banda letu ni pamoja na kufanya udahili hapa hapa kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na programu mbalimbali zinazotolewa na chuo cheti kwa ngazi nilizozitaja.” Alifafanua Sarah

Alisema Mtu anayehitaji kujiunga na chuo hicho, afike kwenye banda la chuo akiwa na picha moja ya passport size ya rangi, na vivuli vya vyeti vya kidato cha nne, (Form Four), na Kidato cha Sita,(Form Six), kwa wale wanaoomba kujiunga na programu za Shahada ya Kwanza, au Cheti cha kuhitimu elimu ya Chuo Kikuu kwa wale wanaotaka kujiunga na programu za Masters.

Akieleza zaidi Sarah alisema, kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na programu za Astashahada (Cheti) wanapaswa wafike na vivuli vya vyeti vya kumaliza elimu ya sekondari (Kidato cha nne) 

Chuo cha Uhasibu Arusha, ni taasisi ya kielimu iliyoanzishwa na sheria ya taasisi za elimu ya uhasibu Arusha ya mwaka 1990 (Act of 1990), udhibiti wa jumla na uongozi wa taasisi uko chini ya Baraza la Uongozi la chuo, (Governing Council), alifafanuaSarah..

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, (NEC), anayeshughulikia masuala ya Siasa na Uhusinao wa Kimataifa, Kanali (mstaafu), Nelubinga, (kulia), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda hilo, huku Afisa Uhusiano na Masoko wa chuo hicho, Sarah Goroi(kushoto), akimsikiliza. Katikati ni Kanali Mstaafu, F.L Kakiziba.
Waziri Dkt. Mpango, akifurahia jambo wakati akipatiwa maeelzo kuhusu huduma za kielimu zitolewazo na Chuo hicho. Kulia ni Afisa Uhusiano na Masoko wa chuo hicho Sarah  Goroi.


Dkt. Mpango, (kushoto), akisaini kitabu cha wageni kwenye banda hilo, wanaoshuhudia kutoka kulia ni Afisa Utawala wa chuo Bi. Sekunde Titus, Afisa Uadahili, Bw.Gerald Malisa, na Afisa Uhusiano na Masoko, Sarah Goroi.

Afisa Uhusiano na Masoko wa chuo cha Uhasibu Arusha Sarah Goroi akitoa maelezo kwa wateja waliofika katika banda lao kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kunakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.

Mngereza kuwa mgeni rasmi tamasha la SHIWATA.

Posted: 09 Jul 2017 12:54 PM PDT

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Geofrey Mngereza amekubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Wasanii litakalofanyika Ijumaa jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib alisema Mngereza atashuhudia michezo mbalimbali itakayofanywa na wasanii na wanamichezo.

Alisema tamasha hilo ambalo awali lilikuwa lifanyike kijiji cha Wasanii Mkuranga limehamishiwa jijini Dar es Salaam sababu kubwa ya kuhamisha tamasha hilo ni kutokana na mvua ya msimu uliopita kuharibu barabara ya kwenda kijijini.

Taalib alisema tamasha hilo sasa litafanyika kwa siku mbili kuanzia Ijumaa Julai 14.7.2017 na kuhitimishwa Jumamosi Julai 15 mwaka huu katika viwanja vya Chuo cha Uhazili, splendid Ilala Bungoni.Alisema mpaka sasa wanatarajia kupokea wanamichezo kutoka sehemu mbalimbali kama vile Mkuranga, Kibiti, Zanzibar na Morogoro ambako zaidi ya wanamichezo 600 wamethibitisha kushiriki.

Baadhi ya michezo ambayo itafanyika ni sarakasi, Tae kwon-do, muziki wa dansi, ngumi, soka,rede,muziki wa asili,wu shuu,ngoma,singeli na michezo mingine.Alisema kampuni ya SBC wanaotengeneza soda za Pepsi imekubali kuwa wadhamini wakuu wa tamasha hilo na kuongeza kuwa milango iko wazi kwa wadhamini wengine kujitokeza.

Akizungumzia ujenzi wa nyumba zao kijijini alisema mgawo na makabidhiano ya nyumba 14 ndogo,kubwa tatu na viwanja 35 vilivyopimwa utafanyika Julai 16 siku moja baada ya kumalizika tamasha hilo.

Alisema kuanzia sasa wanachama wanaotaka kujenga nyumba zao wenyewe wawasiliane na Shiwata ili wapewe maelekezo na utaratibu wa kufanya usafi kwenye makazi yao.Mwenyekiti alisema utaratibu wa kulipia umeme kupitia mpango wa umeme vijiijini (REA)unaendelea na mikakati ya kukarabati barabara ya kufika kijijini unafanyika.

AFYA YA MTOTO MWENGE YAIMARIKA; RC NCHIMBI AWAASA WAZAZI JUU YA KUWAPA WATOTO WAO MAJINA

Posted: 09 Jul 2017 12:52 PM PDT


Afya ya mtoto Mwenge aliyenusurika kifo baada ya kutumbukizwa chooni na kukaa humo kwa zaidi ya saa 14 kabla ya kuokolewa akiwa hai, inaendelea kuimarika huku akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Kiomboi Wilayani Iramba.

Mtoto Mwenge alitupwa chooni na mama yake mzazi Winfrida Lori (23) mwanafunzi katika Chuo cha Uuguzi cha Kiomboi Wilayani Iramba ambapo mama huyo amekiri kujifungua mtoto huyo wa kiume katika Kijiji cha Luono Julai 3, saa mbili usiku kisha kumfunga vitambaa mdomoni na kumtumbukiza chooni.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Kiomboi Regina Alex amesema afya ya Mtoto Mwenge inaendelea kuimarika pamoja na hali ya mama mzazi wa mtoto huyo pia inaimarika tofauti na hapo awali ambapo alikuwa dhaifu na kushindwa kumnyonyesha mtoto.

“Winifrida alikuwa hawezi kumyonyesha mtoto Mwenge hapo mwanzoni lakini sasa hivi anamnyonyesha vizuri na maziwa yanatoka ya kutosha, Mtoto mwenge ana hali nzuri na sasa amefikisha uzito wa kilogramu 2.9 hali ambayo inaridhisha kwakweli”, ameeleza muuguzi huyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (picha ya maktaba).


Serikali Kuimarisha Uwanja wa Ndege wa Mpanda

Posted: 09 Jul 2017 12:44 PM PDT


Serikali imemuagiza Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda kuwasiliana na Kampuni ya Uendelezaji Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO) ili kupata gari la Zimamoto ili ndege za Shirika la ndege Tanzania (ATCL) ziweze kuanzisha safari zake katika Mkoa wa Katavi.

Akizungumza mara baada ya kukagua uwanja huo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amesema kwa muda sasa kiwanja hicho kimekuwa kikitumiwa na ndege chache za Shirika la kuhudumia wakimbizi (UNHCR), hivyo ni wakati sasa kutumika na ndege zetu ili kuboresha huduma za usafiri wa anga Mkoani hapa.

“Kamilisheni mazungumzo na KADCO ili kupata gari la Zimamoto lenye ujazo wa Lita 4,000 litakalokuwa na uwezo wa kukabiliana na majanga ya moto endapo yatatokea, kutakapokuwa na gari hilo uwanjani hapa tutaanzisha safari za ndege za Shirika letu wakati ndege yetu ta tatu itakapowasili,” amesema Eng. Ngonyani.

Aidha, amemtaka meneja wa Uwanja huo wa ndege kuhakikisha anaingiza uwanja huo katika mpango maalum kwa ajili ya ujenzi wa taa kiwanjani hapo ili uwanja huo uweze kutumika kwa mchana na usiku.

Eng. Ngonyani ameongeza kuwa azima ya Serikali ni kuhakikisha usafiri wa anga nchini unaimarika kwa kutumia ATCL na mashirika mengine yalipo nchini hivyo kama Serikali imejipanga kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja ili viwe katika viwango vinavyokubalika.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (katikati) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha ndege cha Mpanda Seth Lyatuu (kushoto) wakati alipokagua huduma za uwanja huo Mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani(Kulia) akikagua Mfumo wa ukatishaji tiketi kwa njia ya kielekroniki katika Stesheni ya Mpanda Mkoani Katavi. Katikati ni Meneja Mradi wa kampuni ya Makgroup Ltd Bw. Joseph Mrosso.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya Reli Tanzania, Kanda ya Tabora Bw. Frederick Masangwa(Katikati), wakati alipokagua huduma za usafiri wa Reli Mkoani Katavi.
Meneja wa Msimamizi wa Bandari ya Kigoma Bw. Morris Mchindiuza (aliyenyoosha mkono) akimwonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia) eneo itakapojengwa bandari ya Kalema iliyopo Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili) akitoka kukagua kingo za bandari ya Kalema iliyopo Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA DSM AMTEMBELEA KARDINAL POLYCARP PENGO LEO

Posted: 09 Jul 2017 12:29 PM PDT

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amtembelea Askofu wa Jimbo kuu Katoliki la Dar es salaam Mwadhama Kardinal Polycarp Pengo Ofisini kwake leo ,Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini leo.baada ya kutoka nje kwa matibabu. 
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akisalimiana na Askofu Mkuu wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinal Polycarp Pengo alipomtembelea ofisini kwake mapema leo.
Askofu Mkuu wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinal Polycarp Pengo akizungumza na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita kuhusu hali ya afya yake alipomtembelea leo Ofisini kwake ,kanisa la Mtakatifu. Joseph.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akimsikiliza Askofu Mkuu wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinal Polycarp Pengo alipomtembelea ofisini kwake leo ,Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini hapa.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akipata Baraka kutoka kwa Askofu Mkuu wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kardinal Polycarp Pengo alipomtembelea ofisini kwake leo, katika kanisa la Mtakatifu Joseph leo alipomtembelea kumjilia hali yake.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kumjulia hali Askofu Mkuu wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama KardinalPolycarp Pengo alipomtembelea ofisini kwake leo, katika kanisa la Mtakatifu Joseph leo alipomtembelea kumjilia hali yake.

Tamasha la E-FM Redio la Komaa Concert lilivyozizima jiji la Mwanza

Posted: 09 Jul 2017 01:04 PM PDT

Tamasha la E-FM Redio ya Jijini Dar es salaam, liitwalo Komaa Concert lililokuwa mahususi kwa ajili ya redio hiyo kuwashukuru wasikilizaji wake wa 91.3 lilifunika jiji la Mwanza kwa mapokezi yao makubwa.Katika tamasha hilo, wanamuziki mbalimbali akiwemo Dulla Makabila, Ney Wa Mitego, Darassa, Stamina, Rich Mavoko, Aga Star, Chemichal, Ben Pol na wengine wengi walidondosha burudani kali katika uwanja wa CCM Kirumba

Darassa akitumbuiza  kwenye tamasha la KOMAA CONCERT uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza

Dulla Makabila akifanya yake kwenye tamasha la KOMAA CONCERT uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza

Ney Wa Mitengo akiwapa raha mashabiki  kwenye tamasha la KOMAA CONCERT uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Picha na BMG


sita wanaodaiwa kuwa ni majambazi wauawa katika majibizano ya risasi na jeshi la polisi

Posted: 09 Jul 2017 12:17 PM PDT

Mwanasoka Ramadhan Shiza Kichuya kutana na kumzawadia shabiki wake nambari moja

Posted: 09 Jul 2017 11:55 AM PDT

Moja kati ya huduma zitolewazo na  Sukos Foundation mbali na Disaster Management pia ni kusaidia familia zisizojiweza. Kwa kulitambua hilo, Bernedicta John akiwa Ni mmoja wa watoto walio na ugonjwa wa saratani ya ngozi ( Skin Cancer) ambae pia anatoka katika Familia ya hali ya chini ( Destitute family) Sukos inashirikiana kumsaidia kijana  huyo pamoja na wengine kama hawa wanaotoka katika familia duni na pia kupata nafasi za kutimiza malengo yao.
Siku ya Leo, baada ya kujua kuwa moja ya ndoto kubwa za Mtoto huyu ni kuwa mchezaji mpira mahiri nchini Tanzania na duniani, na mchezaji anayempenda sana, ama  " Role Model" wake ni mchezaji wa Taifa Stars Na Simba Sports Club Ramadhan Shiza Kichuya. Sukos imefanikiwa  kumkutanisha mtoto huyu namoja na Role model wake Mchezaji Shiza Kichuya ambae amemkabidhi Jezi yenye Jina lake pamoja na kumpa misaada mengine mbalimbali kumsaidia Mtoto huyu anaetoka katika familia duni kutimiza ndoto yake. Hakika Ilikua ni siku ya furaha kubwa sio kwa Sukos pekee bali pia kwa Bernedicta na mwanasoka Ramadhan Shiza Kichuya pia!

DOKTA MPANGO AKUNWA NA MWITIKIO WA WANANCHI KULIPA KODI

Posted: 09 Jul 2017 11:45 AM PDT

Na Benny Mwaipaja, WFM 
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewapongeza Watanzania nchini kote kwa mwitikio wao mkubwa wa kulipa kodi mbalimbali ikiwemo ya majengo kwa hiari, hatua ambayo itaiongezea Serikali uwezo wa kuwahudumia kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dkt. Mpango ametoa pongezi hizo alipotembelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwal. J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Ametoa wito kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa pamoja na kuwahimiza wananchi kudai risiti wanapofanya manunuzi halkadhalika wafanyabiashara kutoa risiti wanapouza bidhaa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Baadhi ya wananchi waliofurika kulipa kodi mbalimbali hususan za majengo katika viwanja hivyo vya Sabasaba, wameeleza kuwa mwitikio na hamasa kubwa waliyonayo ya kulipa kodi inatokana na imani yao kwa Serikali ya Awamu ya Tano jinsi inavyosimamia maendeleo ya nchi kwa umakini mkubwa.
Kwa upande wake Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi Bi. Honesta Nduguru, amewataka Watanzania popote walipo kutumia muda mfupi wa nyongeza uliobaki kulipa kodi badala ya kusubiri dakika za lala salama.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo toka kwa Bi. Honesta Ndunguru, Meneja Huduma kwa Mlipakodi, wa TRA alipotembelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwal. J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Biko yatoa Milioni 10 Tamasha la Komaa Concert la EFM Mwanza

Posted: 09 Jul 2017 12:37 PM PDT


DROO maalum ya kuwania Sh Milioni 10, iliyoandaliwa na waandaaji wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, imeenda kwa kijana mwenye miaka 25, Said Juma, mkazi wa Mwanza, ikitolewa katika tamasha la burudani la Komaa Concert la EFM Radio, lililofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa jana.

Katika tamasha hilo, wasanii mbalimbali wa jijini Mwanza na Dar es Salaam, walipata nafasi ya kutoa burudani kwa mashabiki wao, huku likinogeshwa na Milioni 10 za Biko maalum kwa wakazi wa Mwanza pekee.

Akizungumza katika droo hiyo ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema mshindi huyo alipatikana kwa kupigiwa simu kama wanavyopatikana wengine waliowahi kuvuna mamilioni kutoka kwenye bahati nasibu yao inayochezeshwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa kupitia mitandao ya simu za Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa.

Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kushoto mwenye kipaza sauti, akimtangaza Said Juma kulia, aliyefanikiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni 10 za Biko zilizotolewa maalum kwa ajili ya Tamasha la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio Jumamosi iliyopita na kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Shabiki wa muziki wa kizazi kipya jijini Mwanza ambaye jina lake halikupatikana mara moja akifuatilia onyesho la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio na kudhaminiwa na Bahati Nasibu ya Biko, ambapo pia alitafutwa mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko na Said Juma mkazi wa jijini Mwanza kuibuka kwenye droo hiyo maalum.

Baadhi ya mashabiki wa muziki wa jijini Mwanza, wakiwa katika shangwe kubwa huku mmoja wao akiwa amevaa tshirt ya Biko wadhamini wa tamasha la burudani la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio kwa udhamini wa waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko, ambapo pia ilimtangazaa mshindi wake maalum kwa ajili ya tamasha hilo ambaye ni Said Juma wa jijini Mwanza aliyezoa Sh Milioni 10 za Biko Tamasha hilo lilifanyika jana Jumamosi na kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Alisema kuwa watu waliocheza kwa kufanya miamala kwenye simu zao kuanzia Sh 1000 na kuendelea walichezeshwa kwenye droo moja iliyompa ushindi Juma, huku wakicheza kwa kutumia namba ya kampuni ya 505050 na ile ya kumbukumbu ya 2456.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Zulia Jekundu S1 Ep 130: Wimbledon, Jay Z, Adele, na Lionel Messi

Posted: 09 Jul 2017 09:30 AM PDT

Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima

Posted: 09 Jul 2017 09:26 AM PDT

Watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania wakiwa kwenye banda lao katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam tayari kutoa huduma na maelezo ya shughuli zao. Banda lao limo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango. Kumbuka maonesho hayo yanamalizika rasmi siku ya Alhamisi Julai 13, 2013 hivyo wanakukaribisha uwatembelee.

WAZIRI DKT. MWAKYEMBE AWA MGENI RASMI FAINALI ZA SHINDANO LA BONGO STYLE

Posted: 09 Jul 2017 07:55 AM PDT

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa fainali za shindano la Bongo Style, lililofanyika makumbusho ya Taifa Jijini Dar ,linalohusisha fani za ubunifu wa mavazi,upigaji picha na uandishi wa miswada ya filamu ambapo aliipongeza Taasisi isiyo ya kiserikali ya Faru Arts and Development Organization(FASDO) kwa kuandaa mashindano hayo, alisema kuwa Serikali inalojukumu la kusaidia Asasi kama FASDO ambazo zinaingia katika maswala ambayo Serikali hawakuyawekea msingi mkubwa. "Naomba niagize na kuwa kuna watendaji wetu wa wizara katika sherehe hii mkae chini na watu wa FASDO ili mwaka kesho zoezi hili lifanyikie Bungeni Dodoma" Alisema Dkt. Mwakyembe.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi Agnes Nyahonga  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Goodhope Elieskia maarufu kwa jina la Zagamba  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha uandishi wa miswada ya Filamu
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoMh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa kutoka kulia) akimkabidhi Masoud Masoud  tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda   shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoMh.  Dkt. Harrison Mwakyembe(wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Philip Florian  tuzo ya Best Personality aliyopokea kwa niaba ya Kelvin Mwanasoko ambaye hakuweza fika katika Mashindano hayo.

KIJANA MJASILIAMALI AIOMBA SERIKALI IZITAMBUE BIDHAA ZA MBAO ILI APATE KIWANDA

Posted: 09 Jul 2017 07:43 AM PDT

Na Karama Kenyunko-Globu ya Jamii

, Mjasiliamali anayejihusisha na utengenezaji wa extension za Umeme kwa kutumia mbao, anaiomba Serikali izitambue bidhaa za mbao ili apate kiwanda kikubwa ambacho kitamuwezesha kutoa ajira kwa vijana na bidhaa hizo kufika hadi nje ya nchi.

Charles Antoni Sanga, ambaye ni mwafrica wa kwaza kugundua ujuzi wa kupitisha umeme kwenye mbao, ameongea hayo katika maonyesho ya 41 ya biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Amesema, upitishaji wa Umeme kwenye mbao ni bora na siyo rahisi kusababisha shoti ya Umeme, pia ujuzi huo unatoa fursa kwa kuwainua wajasiliamali wanaochaji simu vibandani.

"Ninahamasidha kauli mbiu ya Mh.Rais kuwa Tanzania ya viwanda inawezekana sababu kuna vitu tunavyobuni watanzania ambayo ni imara kuliko vile vya kutoka nje ya nchi".

Aidha ameiomba Serikali na wadau mbali mbali wanaopenda bidhaa hizo za mbao kujitokeza na kumuinua kwani anafanya kazi katika mazingira magumu kwani hata TBS walimuagiza kuwa awe na karakana na machine Au hata jengo lakini hana chochote kwani hana fedha za kumuwezesha kuwa na vifaa hivyo.

 Mgunduzi wa Soketi ya Mbao Charles Sanga akieleza Kwa Makini jinsi alivoweza kutengeneza Soketi hizo
 Charles Sanga akionesha moja ya Soketi aliyoitengeneza

STAMICO SASA KUMEKUCHA NA MAKAA YA MAWE

Posted: 09 Jul 2017 06:21 AM PDT

· Yaanza kuuza makaa hayo kwa kasi
· Yakiri kuwa na akiba ya makaa ya mawe ardhini ya kuchimba kwa zaidi ya miaka mia moja. 

Na Koleta Njelekela-STAMICO

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeanza rasmi kuuza makaa ya mawe yanayozalishwa katika Mgodi wake wa Kabulo ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wakiwemo viwanda vya saruji na nguo na hivyo kukuza Pato la Taifa.

STAMICO ilianza uzalishaji wa majaribio wa makaa ya mawe katika mgodi wa Kabulo uliopo Kijiji cha Kapeta, Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe mnamo tarehe 30 Aprili 2017 na mpaka sasa imeweza kuzalisha tani 6,197.

Akihojiwa na Mwandishi wa Habari hii, mara baada ya zoezi la uuzaji makaa ya mawe kuanza rasmi huko Kabulo jana (6 Julai 2017), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bwana Hamis Komba, amesema Shirika kupitia mradi wake wa makaa ya mawe wa Kabulo, sasa linaweza kukidhi mahitaji ya watumiaji wote wa makaa ya mawe nchini, katika kipindi cha miaka mia mfululizo kutokana na kuwepo kwa mashapo ya kutosha (mineral resources) na nyenye ubora wa juu katika mgodi huo.

Bwana Komba amesema matarajio ya Shirika ni kuongeza kiwango cha uchimbaji makaa ya mawe kutoka tani 600 hadi tani 1000 kwa siku, hatua ambayo itaiwezesha STAMICO kuzalisha zaidi ya tani 300,000 kwa mwaka. 

“Nchi yetu ina rasilimali nyingi za madini yakiwemo makaa ya mawe, hivyo tunapenda kuwahikishia wenye viwanda vinavyotumia makaa hayo hususani viwanda vya Saruji (Cement), kwamba nchi ina makaa ya kutosha hivyo Serikali haitoshindwa kutosheleza mahitaji na makaa yam awe huku ikitekeleza kwa vitendo azma yake kujenga Tanzania yenye viwanda, ili kukuza uchumi wa Taifa" Alifafanua Bwana Komba.
Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamin Mchwampaka akiwa katika picha ya pamoja na timu wa wataalam wa STAMICO (wanaotekeleza Mradi wa Uchimbaji Makaa ya Mawe-Kabulo) alipotembelea Mgodi huo hivi karibuni kukagua maendeleo ya mradi huo ambao ulianza rasmi uzalishaji makaa yam awe tarehe 30 Aprili, 2017 na kufanikiwa kuzalisha tani 6197 mpaka sasa. Soko la ndani la makaa hayo linawalenga wazalishaji viwandani hususani wale wa viwanda vya Saruji (Cement) na watengenezaji wa nguo, pamoja na magereza na watumiaji wengine wa majumbani.

Shughuli za Uchimbaji Makaa ya Mawe zikiendelea katika mgodi wa Kabulo Kiwira, uliopo katika Kijiji cha Kapeta, wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe. Leseni za Uchimbaji wa Awali wa Madini katika eneo hilo la Kabulo, zina zaidi ya tani milioni 35 zilizothibitishwa za mashapo ya makaa ya mawe, yaliyoko karibu na uso wa ardhi, katika mgodi huo wa Kabulo. Mashapo hayo yanaweza kuchimbwa kwa mfululizo kwa miaka mia moja ijayo.

Mratibu wa Mradi wa Uzalishaji Mkaa ya Mawe wa Kabulo-Kiwira Bwana Alex Rutagwelela ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa STAMICO akielekeza kuhusu zoezi zima la upakiaji makaa ya mawe katika Malori tayari kwa ajili ya kupeleka katika eneo la mauzo lililopo katika kijiji cha Kasumulu, Wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya. Mgodi huo wa Kabulo-Kiwira uliopo katika kijiji cha Kapeta, Wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe unamilikiwa na kuendeshwa na STAMICO kwa niaba ya Serikali.
Malori ya Kampuni ya Lake Cement yakipakia Makaa ya Mawe katika eneo la mauzo ya makaa hayo, lililopo umbali wa kilometa mbili kutoka katika barabara kuu ya Mbeya, iendayo nchini Malawi. Eneo hilo la mauzo lipo katika kijiji cha Kasumulu, Wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya. Makaa hayo ya Mawe yanazalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), katika mgodi wake wa Makaa ya Mawe wa Kabulo, ulipo katika kijiji cha Kapeta, Wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe.

MASAUNI AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYA ZA KONDOA, CHEMBA MKOANI DODOMA LEO

Posted: 09 Jul 2017 05:42 AM PDT

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masaunia kizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kondoa na Chemba mkoani Dodoma. Masauni amefanya ziara ya kikazi katika wilaya hizo. Wa kwanza kushoto  ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota, na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simoni Odunga.Wa kwanza Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani humo, SSP Mohamed Kitia.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, Sezaria Makota wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Wilaya kwa kiongozi huyo ambaye yupo ziarani katika Wilaya ya Kondoa na Chemba. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma, Simon Odunga,wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Wilaya kwa kiongozi huyo ambaye yupo ziarani katika Wilaya ya Kondoa na Chemba. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kondoa, SSP Mohamed Kitia wakati alipokua akitoa taarifa yake ya Ulinzi na Usalama wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota, na Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga. Masauni yupo ziara ya kikazi katika Wilaya hizo ambapo alizitembelea Taasisi zilizopo ndani ya Wizara yake. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MOOVN NA VODACOM KUTOA SULUHISHO LA USAFIRI KUPITIA TEKNOLOJIA

Posted: 09 Jul 2017 05:52 AM PDT

Kampuni  ya Moovn Technologies kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania PLC, wamezindua ushirikiano mpya utakaowarahisishia wateja wao kupata huduma ya usafiri na kuwafikishia huduma za simu watu zaidi ya milioni 12 barani Afrika.


Moovn ni teknalojia inayomwezesha mtu anayetaka usafiri kuupata kwa haraka akiwa sehemu alipo kwa kutumia simu yake ya mkononi au kompyuta. Teknalojia hii pia inawawezesha watu kufikishiwa bidhaa kutoka sehemu mbali mbali na madereva.


Ushirikiano huu kati ya Vodacom ambayo ni moja kati ya makampuni makubwa ya simu za mkononi Afrika pamoja na Moovn, utawawezesha watu zaidi ya milioni 12 kujiunga kwenye huduma hiyo ya Moovn app kwa kupitia simu zao za mkononi.


Kupitia mpango huo, kampuni ya Vodacom itatoa bure au kwa punguzo huduma za data kwa wateja wa Moovn pamoja na madereva ili waweze kupata huduma hiyo kwa urahisi zaidi.Wateja wa huduma hiyo wataweza  kuchagua usafiri wa aina mbali mbali kama vile boda boda, bajaji pamoja na taxi kulingana na mahitaji yao kwa kutumia Moovn app. Pamoja na kulipa kwa fedha taslimu, wataweza pia kulipa kwa kutumia huduma ya kifedha ya M-PesaHuduma hii ya aina yake inalenga kuboresha maisha ya wateja wa kampuni zote mbili zilizo kwenye ushirikiano. Ushirikiano huu pia unalenga kutengeneza ajira pamoja na kuboresha hali ya kiuchumi kwa jamii za Kitanzania na Afrika kwa ujumla.“Tunayo furaha kuungana na mshirika mwenzetu katika kutoa huduma hii muhimu tukilenga kwa pamoja  kubadili maisha ya watu,” anasema Godwin Gabriel ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa MoovnKumhakikisha mteja usalama wake, mtumiaji wa huduma hii anaweza kubonyeza batani inyoitwa ‘panic button’ na ujumbe mfupi wa maandishi utatumwa kwa mtu wake wa karibu ukieleza sehemu alipo na utambulisho wa dereva muda wowote wakati akiwa kwenye chombo cha usafiri.Kipengele hiki cha usalama ni muhimu kwa kuwa kwa siku za hivi karibuni kumekuwa  na matukio ya abiria kufanyiwa uhalifu na baadhi ya madereva wasio waaminifu. Mteja pia anaweza kuwafamisha ndugu jamaa na marafiki zake kinachoendelea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa safari yake.Pamoja na mambo mengine, huduma hii itawawezesha wafanyabiashara kufuatilia bidhaa na huduma wanazowapelekea wateja wao kuanzia wanapomkabidhi dereva hadi zinapomfikia mteja.Madereva  watakuwa wakipata malipo yasiyobadilika (Flat commission) kwa kila safari watakokuwa wakifanya na  kwa upande wao wateja watafurahia gharama zisizopanda.Naye Mkurugenzi wa kitengo cha biashara wa Vodacom Hisham Hendi alisema “M-Pesa inawawezesha watu wote kuweza kufikiwa na huduma ya kifedha kwa urahisi katika sehemu walipo. Wakati tukifanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa watanzania wengi wanafikiwa na huduma za gharama nafuu za kifedha, tunaendelea pia kuwaletea wateja wetu huduma zenye ubunifu zinawezesha Serikali na biashara kuwasiliana huku tukitoa malipo mazuri kwa mawakala wetu,”Aliwashauri watumiaji wa mtandao huo kwa kufanya malipo kwa njia ya simu kwani ni salama zaidi kuliko kubeba fedha taslimu. Kupitia huduma ya LIPA KWA M-PESA alisema malipo katika huduma nyingi na bidhaa yamerahisihwa kupitia App mpya ya M-Pesa

WAZIRI MWAKYEMBE APAMBA MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA DAR GYMKHANA

Posted: 09 Jul 2017 05:22 AM PDT


Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana (DGC) ambayo ni miongoni mwa klabu kongwe za michezo hapa nchini Tanzania, leo imeadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake kwa mtindo wa aina yake uliowakutanisha wadau mbalimbali wa klabu hiyo kupitia chakula cha jioni jijini Dar es Salaam.

Tangu wiki iliyopita, kumekuwa na shughuli mbalimbali za kimichezo ambazo zilianza kufanyika tangu 3 Julai na kilele chake kuwa siku ya leo ya tarehe (08/07/2017). Shughuli hizo ziliandaliwa kwa lengo la kupamba tukio hili muhimu.

Miongoni mwa michezo iliyokuwa ikifanyika ni pamoja na tenisi, kriketi, squash, mashindano ya gofu na michezo mingine mingi.

Mgeni rasmi aliyehudhuria sherehe ya kilele cha maadhimisho hayo wakati wa kufunga michezo hiyo, alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ambaye alizungumiza shamrashamra za kuadhimisha miaka 100 ya klabu hii mkongwe.

“Binafsi nimefurahishwa sana kusikia kwamba michezo yote iliyohusishwa kwenye maadhimisho ya tukio hili kubwa na muhimu ambalo imefanyika na kuisha salama kwa kipindi chote cha wiki moja, jambo ambalo linaonyesha waandaaji walijapanga vyema. Ni imani yangu kwamba udhamini wa wadau mbalimbali umewezesha kufanikisha kufanyika michezo yote hii muhimu,” alisema Waziri Dk Mwakyembe.

Dk Mwakyembe alisema matarajio ya serikali ya awamu ya tano ni kuona wadau wanaongeza nguvu kujihusisha zaidi kwenye shughuli za michezo jambo ambalo linaweza kuibua vipaji zaidi kwa Watanzania wote.

Waziri Mwakyembe alimwaga pongezi kwa wanachama wote wa klabu hiyo wa sasa na wale waliopita pamoja na kila mtu ambaye alishiriki kwa nafasi yake kuhakikisha klabu ya Dar Gymkhana inafanikiwa zaidi.

“Ninatambua fikaumuhimu wa klabu hii kwa ngazi ya taifa letu kwani imekuwa miongoni mwa taasisi ambayo imekuwa ikihamasisha kukuza michezo, utalii na kuwakutanisha pamoja watu kwenye matukio ya kijamii,” alisema.

Waziri Mwakyembe aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kushiriki michezo mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha afya zao na kuwahamasisha wananchi kujiunga na klabu hii ambayo ina michezo mbalimbali. Alisema klabu hii imekuwa ikiwakutanisha wageni kutoka mataifa mbalimbali na Watanzania.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikabidhi kikombe kwa Nahodha wa mpira wa miguu wa Klabu ya Gymkhana Aliabid Mamdani (kulia) baada ya timu yake kuibuka washindi wa jumla katika michuano iliyofanyika hivi karibuni katika kuadhimisha ya miaka 100 ya klabu ya Gymkhana. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana wakati wa kilele cha maadhimisho hayo jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Mwenyekiti wa klabu ya Gymkhana Walter Chipeta.
Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya Klabu ya Dar es salaam Gymkhana yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakeyembe akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya Klabu ya Dar es salaam Gymkhana yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Dar Gymkhana, George Kritsos wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 100 ya Klabu ya Dar es salaam Gymkhana yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. 


NDOTO YA MWALIMU YATIMIA, LUGHA YA KISWAHILI LULU YA AFRIKA

Posted: 09 Jul 2017 05:12 AM PDT

Na Judith Mhina - MAELEZO

Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni muasisi aliyeenzi lugha adhimu na tamu ya Kiswahili na anastahili tuzo maalum kwa kutambua umuhimu wa lugha  hiyo katika kuleta umoja, mshikamano, na maendeleo barani Afrika.

Mwalimu kwa kutambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili, alianza kuweka mfumo wa matumizi ya lugha hiyo katika utendaji wa serikali, jamii nzima ya Tanzania na Umoja wa Afrika. Aidha, sera za Tanzania za kushiriki katika kupigania Uhuru wa nchi kadhaa za Afrika na uwepo wa wakimbizi nchini kwa idadi kubwa imewezesha lugha hii kuvuka mipaka na kuenea kote kusini mwa Afrika.

Mwalimu amepata wapiganaji mahiri wa lugha ya Kiswahili ambao wapo wengi, lakini kwa uchache makala yangu itaangazia viongozi yaani, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi, na Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano, Marais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, Rwanda, Paul Kagame, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila na Jemedari wa kuenzi lugha ya Kiswahili anayeifanya lugha hii kuwa Lulu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli. 

Mtakubaliana nami mchango wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi katika kutumia lugha ya Kiswahili fasaha, katika shughuli zote za Serikali na za kijamii zilisukuma mwamko wa gurudumu la kiswahili kusonga mbele haswa kwa wale wanaodhani lugha za kigeni ni bora kuliko lugha yao.

MICHUZI TV: MAK BAND WANOGESHA USIKU WA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA MY WEDDING SOLUTIONS

Posted: 09 Jul 2017 04:57 AM PDT

5.24Score
3 Hearts
mark Beautiful

Email Newsletter

Sign up for our email newsletters

Facebook Page

Twitter Page

Recent Post

Tags